LISHE: Jinsi ya kuandaa 'githeri' cha mahindi na mbaazi
Na DIANA MUTHEU
MCHANGANYIKO wa mahindi yaliyopikwa pamoja na maharagwe au punje za kunde au mbaazi aghalabu huitwa pure lakini watu wengi nchini Kenya wanaita ‘githeri’.
Muda: Saa 1 dakika 30
Vinavyohitajika
Mahindi mabichi 4
Mbaazi 1/4
Nyanya 2
Dania (fungu 1)
Kitunguu 1
Pilipili mboga 1 (ndogo)
Kitinguu saumu (vipande 2)
Pilipili ya kawaida (kichaa) (sio lazima)
Mafuta (vijiko viwili vikubwa)
Sufuria
Jinsi ya kuandaa
Chemsha mchanganyo wako wa mahindi mabichi na mbaazi kisha pika na uhakikishe kuwa chakula hiki hakina maji kabisa. (Waeza mwaga maji yaliyobaki)
Katika sufuria safi, pika kitunguu kwa mafuta yako hadi kiive vizuri kisha uongeze nyanya, pilipili mboga, chumvi ya kutosha, na kitunguu saumu ulichokiponda vizuri. Funika na uache kwa muda wa dakika tatu hadi ili upate ‘supu’.
Katika supu hiyo ya nyanya, ongeza mahindi na mbaazi na ukoroge vizuri kisha uache iive kwa dakika mbili. Sasa ongeza dania yako, koroga na upakue chakula kingali moto.
Furahia.
Waeza andaa pamoja na parachichi. Pia kama hupendi vyakula vya kukaangwa, waeza pakua mchanganyiko wako wa mahindi na mbaazi baada tu ya kuchemsha.