Makala

MAPISHI NA UOKAJI: Keki yenye mdalasini

June 7th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MUDA wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa kuoka: Dakika 40

Walaji: 5

Vinavyohitajika

· unga wa ngano vikombe viwili

· kijiko 1 cha baking powder

· vijiko 2 vya mdalasini

· kijiko ¾ cha chumvi

· vijiko 8 vya siagi

· sukari kiasi cha vikombe viwili

· kijiko 1 cha vanilla extract

· mayai 3

· kikombe 1 cha maziwa

Keki ya mdalasini. Picha/ Margaret Maina

Maelekezo

Washa ovena na dhibiti nyuzijoto 175.

Paka siagi kwenye chombo cha kuokea keki na uweke pembeni.

Kwenye bakuli kubwa, changanya unga wa ngano, mdalasini, chumvi na baking powder kisha weka kando.

Kwenye bakuli lingine, saga sukari na siagi mpaka ilainike vizuri. Ongeza mayai huku unachanganya. Koroga mpaka ilainike vizuri kisha weka vanilla. Changanya vizuri.

Ongeza mchanganyiko wa unga wa ngano kidogo kidogo huku ukichanganya na maziwa. Koroga hadi uchanganyike vizuri.

Mimina mchanganyiko wako kwenye chombo cha kuokea ulichopaka siagi awali.

Oka keki kwa dakika 45. Ikiiva, acha ipoe kisha hamishia keki kwenye sahani.

Toboa toboa au dunga kwa kijiti safi wakati bado ingali moto kiasi.

Changanya sukari, maji, siagi, mdalasini na vanilla. Koroga mpaka siagi na sukari viyeyuke vizuri

Mwagilia juu ya keki na upakue.

Furahia na juisi, maziwa au chochote upendacho.