Makala

MAPISHI: Queencakes zikiwa na ndizi

April 19th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

MUDA wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa kuoka: Dakika 40

Walaji: 4

Queencakes. Picha/ Margaret Maina

Vinavyohitajika

–          Unga wa ngano vikombe 2

–          Baking soda kijiko 1

–          Baking powder kijiko 1

–          Chumvi ½  kijiko

–          Ndizi 3 kubwa zilizoiva vizuri

–          Buttermilk vijiko 3

–          Maziwa vijiko 3

–          Yai 1

–          Vanilla ¼ kijiko

–          Nutmeg ½  kijiko

–          Sukari ¾ kikombe

–          Mdalasini ¼  kijiko

–          Butter vijiko 5 au Blueband

Maelekezo

 

–          Pasha ovena nyuzijoto 190°C,

–          Chukua bakuli, weka unga, baking soda, baking powder, chumvi, nutmeg kisha changanya vizuri

–          Yeyusha siagi. Menya ndizi na uvikate vipande vidogo vidogo,ongeza sukari, maziwa, buttermilk na yai kisha anza kuziponda.

–          Ongeza siagi na uchanganye vizuri.

–          Chukua mchanganyiko wenye ndizi changanya kwenye ule wenye unga, kisha anza kukoroga uchanganyikane wote kwa pamoja.

–          Kisha chukua bakuli lingine, weka sukari vijiko viwili vya chai, unga vijiko viwili vya chakula, mdalasini na butter changanya vizuri.

–          Kisha weka mchanganyiko huo kwenye mchanganyiko ule wa unga.

–          Tumia kijiko kuweka mchanganyiko kwenye karatasi ya queencakes

–          Kisha weka kwenye chombo cha kuokea na uoke kwa dakika 40

–          Ikishakuwa na rangi ya kahawia, epua.

Acha vipoe kabla ya kupakua na juisi au maziwa.

Furahia.