MAPISHI: Ugali na sukumawiki
Na MARGARET MAINA
UGALI
Muda wa kusonga sima: dakika 15
Walaji: 2
Vinavyohitajika
– Unga wa mahindi nusu kilo
– Maji lita 1
Maelekezo
Mimina maji kwenye sufuria kisha bandika kwenye meko ili yachemke.
Tengeneza mchanganyiko kwa kuongeza unga kiasi kwenye maji yanayochemka huku ukikoroga.
Ongeza unga ukikoroga kwa mwiko hadi uwe mgumu.
Endelea kukoroga ukihakikisha hakuna mabonge ya unga hadi ugali uwe laini.
Punguza moto kisha funika ugali kwa dakika 10.
Epua na upakue.
Sukumawiki
Muda wa kupika: Dakika 5
Walaji: 2
Vinavyohitajika
– Sukumawiki
– Pilipili kijiko 1
– Chumvi kijiko 1
– Maziwa vijiko 4
– Kitunguu
– Pilipili mboga
– Mafuta ya kupikia
– Kitunguu saumu kijiko 1
Maelekezo
Andaa kitunguu na pilipili mboga kwa kukata vipande vidogovidogo.
Andaa sukumawiki.
Bandika sufuria mekoni hadi ipate moto. Weka mafuta kisha weka sukumawiki. Koroga vizuri kisha funika na uache kwa dakika moja kisha koroga na uepue.
Kwenye sufuria nyingine, weka mafuta kisha kitunguu maji. Koroga, weka kitunguu saumu, pilipili na chumvi. Endelea kupinduapindua.
Weka pilipili mboga, koroga na uache kwa dakika mbili vichemke pamoja.
Weka sukumawiki, koroga vizuri kisha weka maziwa na uache ichemke kwa dakika 3 kisha epua.
Pakua na ugali na ufurahie.