Makala

Pandashuka za Balozi Amina Mohamed ndani ya serikali ya UhuRuto

March 1st, 2019 Kusoma ni dakika: 5

Na MWANGI MUIRURI na GEOFFREY ANENE

RAIS Uhuru Kenyatta katika mabadiliko katika baraza la mawaziri wake amemhamishia Balozi Amina Mohamed kutoka wizara ya Elimu hadi kwa ile ya Spoti na masuala ya Vijana.

Ni hatua ambayo katika udadisi wa kitaaluma haionekani kuwa na mwelekeo wowote ila tu wa kumhifadhi ndani ya baraza la mawaziri kwa kuzingatia mengine kando na utendakazi wa uhakika kwa Wakenya.

Lakini akiwa Waziri wa Elimu ambapo amehamishwa na nafasi yake kujazwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani (KNEC), Prof George Magoha, alijulikana na kuwa na utendakazi baridi na moto, akitangaza sera hii leo mchana, usiku  anabadilisha na kutangaza sera kinyume au tofauti kabisa.

Ni hali ambayo ilimpata akichanganya wadau wote wa elimu kuhusu mfumo mpya wa elimu, kuhusu sera ya vitabu katika mtaala mpya na pia sera kuhusu usajili wa wanafunzi katika kidato cha kwanza.

Alijishindia ushabiki alipoamrisha wakurugenzi wa elimu Desemba 2018 wafanye uchunguzi wa sababu za wanafunzi kutungwa mimba kinyume na sheria ikizingatiwa kuwa ni makosa makuu katika sheria za Kenya kushiriki ngono na mtoto.

Alisema kuwa habari za wengi wa watoto wasichana katika darasa la nane kufanyia mitihani katika wadi za kina mama kujifungua ni ushahidi tosha wa jamii ambayo imepotoka kimaadili kiasi kwamba iko na wanaume ambao wanashiriki ngono na watoto hali ambayo aliitaja kuwa ya kuwafanya watoto kuwa walezi wa watoto.

Aidha, alipinga vikali wito wa adhabu ya kiboko kurejeshjwa shuleni, akisisitiza kuwa hata akipokezwa sheria hiyo kutoka bunge hangeitekeleza, akisema kuwa ni adhabu ya kuhujumu haki za kibinadamu hasa zile za watoto.

Alishikilia kuwa kuna njia nyingi za kurekebisha tabia za watoto pasipo kuwacharaza viboko akiitaja adhabu hiyo kama iliyopitwa na wakati.

“Kinyume na maoni hayo ya kutumia kiboko kurekebisha tabia za watoto, kuna njia nyingi za kisasa ambazo zinaweza zikatumika. Kiboko hakitawafanya watoto hawa wakome kuchoma mashule na hatuzingatii kama serikali kutumia njia ya mkato ambayo imepitwa na wakati,” akasema Bi Mohamed.

Ingawa kuna wanaojua kuwa Bi Mohamed ndiye mama mzazi wa Firyal Nur Al Hossain ambaye ndiye mchumba wa mwanaye Rais, Jaba Muhoho, haijulikani kama Rais alizingatia utendakazi wa waziri huyu au ushemeji.

Awamu ya kwanza

Hata hivyo, Bi Mohamed alionekana kung’aa katika awamu ya kwanza ya utawala wa UhuRuto kati ya 2013 na 2017 ambapo alikuwa Waziri wa Masuala ya Kigeni, wadhifa ambao alipokonywa katika awamu ya pili ya UhuRuto na ukakabidhiwa Bi Monicah Juma, ambaye ni mkewe mshauri wa kisiasa wa Rais Kenyatta, Prof Mwangi Kagwanja.

Bi Mohamed alizaliwa mnamo Oktoba 5, 1961, hivyo basi kumfanya wa rika moja na Rais Kenyatta.

Akiwa wakili kitaaluma, ndiye mwanamke wa kwanza nchini kuwa Waziri wa Masuala ya Kigeni na pia wa kwanza mwanamke duniani kuwa mwenyekiti wa kamati ya General Council of the World Trade Organisation, Dispute Settlement Body, International Organisation for Migration na pia Rais wa United Nations Office for Drugs and Crime.

Bi Mohamed alisomea shule ya msingi ya Township katika Kaunti ya Kakamega kabla ya kujiunga na ile ya upili ya Butere Girls, kisha ile ya Highlands akijiandaa kujiunga na Chuo Kikuu cha Kiev nchini Ukraine.

Alihitimu na shahada ya Sheria na kisha akahitimu kwa nyingine ya uzamili kuhusu sheria ya kimataifa na pia akajipa shahada  nyingine kuhusu sheria nchini Kenya katika Kenya School of Law na pia Stashahada katika somo la husiano za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Oxford.

Mwaka wa 2006, Bi Mohamed aliteuliwa kuwa mjumbe maalum katika uhusiano wa Kenya na Muungano wa Bara Ulaya (EU) na pia afisa mkuu wa masuala ya Wakenya walio ng’ambo.

Alikuwa tayari ametangaza nia yake ya kupunguza  ada zinazotozwa watahiniwa wa kibinafsi wanaolenga kufanya mitihani ya kidato cha nne (KCSE) na darasa la nane (KCPE) akisema kuwa ada hizo ni kisiki cha kuafikia elimu kwa wote.

Alikuwa ametangaza kuwa angewasilisha pendekezo katika baraza la mawaziri ili kuundwe sera ya kupunguza ada hizo alizozitaja kuwa hazifai taifa linalolenga kuafikia malengo ya kielimu.

Bi Mohamed alisema kuwa kwa sasa watahimiwa wa kibinafsi wa KCSE hulazimika kutoa Sh5,500 kwa tume ya usimamizi mitihani nchini (NEC) na ada nyingine ya Sh3,000 kwa kituo cha kufanyia mtihani huo hivyo basi kujumlisha gharama hadi Sh8,500.

“Nao wale wanaolenga kufanya mtihani wa KCPE wakijifadhili hulazimika kulipa Sh800 kwa NEC na hatimaye Sh1, 200 kwa kituo cha kutahiniwa hivyo basi kujumlisha gharama hadi Sh3,000. Huo sio mfano bora wa kushawishi wengi ambao wangetaka kufuatilia ndoto zao kuhusu elimum kufanya hivyo bali ni kikwazo kikuu,” akasema akiwa katika Kaunti ya Kiambu kuratibu mikakati ya kushirikisha mtihani wa KCPE 2018.

Alisema kuwa ada hizo ni kero kuu kwa wale wazima ambao wanatia bidii ya kujua kusoma na kuandika na pia wale wengine wa ujana ambao kwa sababu moja au nyingine hawakuafikia utaratibu wa kukalia mitihani hiyo sambamba na watahiniwa wanaofadhiliwa na serikali.

Mwaka wa 2008 ndiye huyo Bi Mohamed akawa Katibu maalum katika wizara ya haki, katiba na uwiano wa kitaifa.

Akiwa na tuzo kadha za kitaifa kutoka afisi ya rais na kwingine katika huduma ya uongozi, Bi Mohamed ameolewa na Khalid Ahmeda mbapo wana watoto wao wawili huku pia wakilea wengine wanne ambao ni mayatima.

Mwaka 2018, Bi Mohamed aliandaa karamu katika Kaunti ya Kakamega katika hali ambayo iliashiria anajiandaa kujitosa katika ulingo wa kisiasa mwaka wa 2022 na ambapo anatajwa kama anayelenga ugavana baada ya kung’atuka kikatiba kwa Wycliffe Oparanya.

Mitandaoni

WAZIRI mpya wa Wizara ya Michezo, Amina Mohammed amekaribishwa katika wizara hii yake ya tatu tangu mwaka 2013 kwa kejeli.

Inaonekana watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii hawaamini Amina atafanya kazi nzuri katika Wizara ya Michezo.

Amina amejaza nafasi ya Rashida Echesa Mohamed, ambaye amepigwa kalamu na Rais Uhuru Kenyatta mnamo Machi 1, 2019.

Baada ya uteuzi wa Amina kutangazwa, sehemu kubwa ya Wakenya haikuridhishwa na waziri huyu wa zamani wa Wazara ya Masuala ya Kigeni na Wizara ya Elimu.

Haya hapa maoni ya baadhi ya Wakenya waliosikitishwa na Amina kuwasili katika Wizara ya Michezo. Maoni yao yamefanyiwa mabadiliko machache sana.

Karugu Mureithi: Now that is progress. But Amina is also a failure. She will run down sports.

Wamahiu Njogo: (Rais Uhuru Kenyatta) Ameona pia Amina ako na mchezo mwingi akaona she fits well in the sports docket.

Carol Kui: Nilisema tu Amina ako na mchezo mingi sana.acha akachezee hukooo uwanjani wa sport lakini sio uwanja wa masomo.

Hinga Hinga: Amina ako na mchezo sana acha aende tuu uko! (Aende tu huko).

Killy Emmanuel: Sports ministry has been a dumping site for failed cabinet secretaries, as a sportsman I’m so disappointed. (Wizara ya michezo imekuwa ni dampo la kila aina ya takataka).

Kingori Alice: I’m happy for the education sector. Amina played too much. Ninafurahi kwa sababu Amina alifanya kazi nzuri katika sekta ya elimu).

Charity Nyambura: Finally Prof Magoha, the change we needed as parents. Amina can go to slay in sports. (Hatimaye Prof Magoha; mabadiliko tuliyoyataka).

Vg Wambui: Hiyo mchezo Amina alikuwa nayo lazima angemalizia ministry of sports akacheze sports pesa huko.

Leon Gitobu: Rashid Echesa the now sacked sports minister never went beyond standard 8, however that did not deter him from becoming what he aspired to be. My blame goes to the President for appointing him knowing very well he was doomed to fail. Amina is a diplomat and I don’t think the sports ministry is suitable for her either.

Sammy Omurwa: Prof. Magoha can make a great and good change in Education ministry, Amina can’t make it in sports, l think she belongs at the ministry of Foreign affairs

Geff Scotfield: Amina ameonekana ako na mchezo sana akarushwa sports…..go on and hunt sportpesa defaulters nobody can stop reggae.

Dk Wa Thindigua: Vile Amina alionekana ako na mchezo katika elimu ndivyo Uhuru amempeleka wizara ya michezo!

Tamey Izzo: Wacha Amina apeleke hiyo mchezo ya HELB ministry of sports. She was better off as a diplomat.

David Kamau: CS AMINA ALIKUWA NA MCHEZO SANA NO WONDER AMEPELEKWA SPORTS AKACHEZE PROPER.

Mbegra Josh Eldest: Hiyo ni sawa. Amina Mohammed anakuanga na mchezo sana.

Pst Gideon Kurgat: Kenya surely!!! We are expecting the arrest of corrupt ministers instead of reshuffle and sacking!!! Again Amina is not fit for sports at all!! She should think twice before taking the role, imagine from Foreign Affairs to Education then finally to sports!!! Abnormal!! (Hii Kenya ni nchi isiyoisha vituko. Tulichotarajia kilikuwa ni kukamatwa kwa mawaziri mafisadi na wala sio mabadiliko na kufutwa kwa baadhi. Amina hafai katika Wizara ya Michezo. Alifikirie hili kabla ya kuhama kutoka Wizara ya Elimu hadi ya michezo. Hebu fikiri kutoka Wizara ya Masuala ya Kigeni hadi ya elimu na sasa ya michezo!)

Flora Biwott: Amina was good in foreign ministry. Sports docket is for young and energetic people. (Amina alifanya vizuri katika wizara ya masuala ya kigeni. Hii ya michezo inahitaji kijana mwenye kuchacharika kabisa).

Calleb Njega: Amina alisomea nini??? Kila ministry??? Hakuna mwenye alicheza ambaye ana tajiriba was kuongoza michezo??? Naumwaa sana.

Echesa, ambaye watumiaji wa mitandao ya kijamii wanasema alijichimbia kaburi alipoitisha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga amfute kazi na pia kuhusishwa katika sakata ya ulanguzi wa wanawake kutoka Pakistan mnamo Januari mwaka 2019 na pia kuwa na kiwango cha chini cha masomo, pia hakupata mapokezi mazuri kutoka kwa sehemu kubwa ya Wakenya.