Shangazi Akujibu
Mtoto niliyepata kabla ya ndoa anateseka, nitamchukuaje?
SWALI: Mpenzi wangu aliniacha akaolewa na mwanamume mwingine. Mumewe hana kazi kwa sasa na wanaishi kwa shida. Tulikuwa tumezaa pamoja na nahisi vibaya mtoto wangu akiteseka. Nafikiria kumchukua. Nishauri.
Jibu: Mpango huo utahitaji mazungumzo na maelewano. Ingawa mtoto huyo ni wako kumzaa, sasa ana baba mwingine. Jaribu kushauriana nao bila kugusia hali yao. Itabidi pia uzungumze na mke wako ili amkubali mtoto huyo.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO