Shangazi Akujibu

Nilikuwa kahaba ila sasa nimebadilika nitoe siri?

August 7th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

NILIKUWA kahaba kwa miaka mitano lakini sasa nimebadilika na kupata mpenzi wa kweli. Nimeficha historia yangu. Je, ni lazima nimfichulie?

Kila mtu ana historia yake, lakini si kila historia inahitaji kutangazwa. Ikiwa maisha yako ya sasa ni mapya na umebadilika kweli, basi tafakari kwa makini kabla ya kufichua.

Simpendi mume wangu, nivumile ndoa au niondoke?

Nina miaka mitatu katika ndoa lakini sijawahi kumpenda mume wangu. Niliolewa kwa sababu ya shinikizo la wazazi. Je, niendelee kuvumilia au nitafute furaha yangu?

Kuendelea kuishi maisha yasiyo na furaha ni kujitesa. Thamani yako iko juu kuliko kuvumilia mateso kwa jina la ndoa.

Nimeshindwa kusahau mpenzi wa kitambo

Nimeshindwa kabisa kumsahau mpenzi wangu wa zamani. Kila ninapoingia kwenye uhusiano mpya, huwa naanza kumlinganisha wa sasa na huyo wa zamani. Ningependa sana kuanza maisha upya ila sijui nifanyeje. Naomba ushauri.

Unafaa uchukue muda kabla ya kukimbilia mahusiano mapya. Chukua muda wako, jielewe na jipende. Mapenzi mapya hayawezi kustawi ikiwa una kumbukumbu kama hizo.

Shogangu ana mpenzi wa nje, nimwambie mumewe?

Nimegundua kuwa rafiki yangu wa karibu ana mpenzi wa nje, na mume wake hajui. Je, ni wajibu wangu kumwambia ukweli au?

Ikiwa una uhusiano wa karibu naye, jaribu kwanza kuzungumza naye kwa upole. Kumshtaki kwa mume wake moja kwa moja kunaweza kukuingiza kwenye mgogoro wa ndoa yao.