Shangazi Akujibu
Nipe Ushauri: Nimepata binti mrembo na shupavu chumbani, shida yake ni ulevi

Hujambo Shangazi?
KUNA huyu binti ambaye nilikutana naye wiki mbili zilizopita. Nampenda sana hasa ikizingatiwa kwamba yeye ni shujaa sana chumbani. Lakini tatizo ni kwamba analewa sana. Nifanyeje?
Sijambo!
Kwanza kabisa, wiki mbili ni muda mfupi sana kumfahamu mtu. Kisha, unapaswa kujua kwamba kuna mambo mengi muhimu maishani kando na ustadi wa chumbani. Sawazisha mambo haya kisha ufanye uamuzi wake.