NIPE USHAURI: Fimbo yake ndogo sana inapotelea kisimani
NILISHIRIKI burudani na mume wangu kwa mara ya kwanza juzi baada ya kufunga ndoa. Nimegundua hali ambayo sikutarajia; kifaa chake ni kidogo sana hakiwezi chochote. Nimeamua kumuacha.
Kama shughuli hiyo ni muhimu kwa maisha yako ya ndoa, itakuwa vigumu kuishi na mume wako. Itabidi ushauriane naye kuhusu uamuzi wako kisha umhakikishie hiyo itabakia siri yenu tu.
Mume alitoroka na meidi sasa amemuoa
Nina mume na watoto wawili. Mwezi jana mzee alitoweka na mfanyakazi wetu wa nyumbani. Baadaye alinipigia simu akaniambia huyo sasa ndiye mke wake. Ameahidi kugharamia mahitaji yetu na watoto.
Uhusiano wa kimapenzi na ndoa hutokana na hiari. Iwapo mume wako ameamua hataki ndoa kati yenu, huwezi kumlazimisha. Kubali uamuzi huo na uendelee na maisha yako.
Mistari ya kuingiza demu boksi imenikaukia
Nina umri wa miaka 23. Marafiki zangu wote wana wapenzi lakini mimi sina. Tatizo ni kuwa sijui kuzungumza na wasichana. Nifanyeje?
Sidhani hilo hasa ni tatizo kwako. Kama unajumuika na kuzungumza na marafiki zako wa kiume, inaweza kuwa hivyo kwa wasichana. Na iwapo hutangamani na wasichana, itabidi uanze ndipo ujue kuzungumza nao.
Mpenzi anadai mahaba ninayompa hayatoshi
Nina rafiki ameniambia mpenzi wangu amekuwa akitaka wawe na mpango wa kando kwa sababu simtoshelezi kimapenzi. Habari hizo zimenichoma vibaya moyoni.
Hakuna mwanamume anayependa kuhusishwa na upungufu wa aina hiyo. Mpenzi wako aliona aibu kukwambia na alijua utaumia moyoni. Sasa umejua. Shauriana naye kuhusu mwelekeo wa uhusiano wenu.