Shangazi Akujibu
Posho langu limekatwa sasa mke ananinunia
PICHA | HISANI
SWALI: Mwajiri wangu amepunguza mshahara wangu kutokana na hali ngumu ya kiuchumi na nimelazimika kupunguza matumizi nyumbani. Mke wangu hana raha kutokana na hatua yangu hiyo. Nifanye nini?
Jibu: Uchumi umeharibika na jinsi moja ya kukabiliana hali hiyo ni kupunguza matumizi ya nyumbani. Kama hukumshauri mke wako kuhusu hatua yako hiyo, itakuwa vyema uketi naye chini umwelezee.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO