Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Ananiaibisha mbele ya marafiki
SWALI: Vipi Shangazi? mume wangu anapenda kuniaibisha mbele ya watu. Huwa anafanya nihisi mjinga sana mbele ya marafiki zake. Nachukia hiyo tabia yake. Nifanyeje?
Jibu: Huo ni unyanyasaji wa kihisia. Ongea naye faraghani na uweke mipaka kuhusu suala hilo. Aibu hadharani huharibu heshima na mapenzi. Unapokuwa katika hali ya kukosa raha yeye pia afaa kuhisi vivyo hivyo kwa sababu yeye ni mpenzi wako wa kweli.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO