Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Mume humbagua mtoto niliyezaa kabla ya ndoa
Mama mjamzito. PICHA|HISANI
SWALI: Kwako shangazi. Niliolewa nikiwa na mtoto kutokana na uhusiano wa awali. Mume wangu aliahidi kumpenda kama wake. Lakini anaonekana kupendelea wawili ambao tumezaa pamoja na hilo linaniumiza moyoni. Nishauri.
Jibu: Mume wako amekiuka ahadi yake kwako. Unafaa umkumbushe na kumwelezea unavyohisi unapoona akimbagua mtoto wako. Kama hatajirekebisha, uko huru kuondoka badala kuendelea kuona mwanao akiteseka.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO