Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Mume sasa anashuku nimepata mtoto wetu nje ya ndoa!
SWALI: Kuna jambo linatishia kuvunja ndoa yangu. Mume wangu anashuku kuwa mtoto wetu wa pili si wake na amekuwa akisisitiza kujua baba yake. Sijawahi kwenda nje ya ndoa na nina hakika ni wake. Nifanye nini?
Jibu: Sijui mume wako ametumia kigezo gani kufikia uamuzi kwamba mtoto huyo ni wa mtu mwingine. Mnaweza kuthitbitisha ukweli kupitia ukaguzi hospitalini. Mwambie mwende mkapimwe ili kumaliza ugomvi.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO