Makala

SIHA NA LISHE: Kiamshakinywa

September 5th, 2019 Kusoma ni dakika: 2

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KIAMSHAKINYWA ni chakula cha kwanza cha kila siku, ambacho mtu hula baina ya alfajiri na dakika chache kabla ya mchana.

Kulingana na pendekezo la wataalamu wa lishe, ni chakula ambacho mtu hafai kuruka kwa sababu ya umuhimu wake.

Watu ambao wanasahau kupata kiamshakinywa wana uwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya kiwango cha sukari, kunenepa sana, au mshtuko wa moyo.

Chakula cha kwanza kinaweka safu kwa siku nzima, husaidia mwili na viungo kuwa ange kabisa na kuamsha michakato ya metaboli.

Staftahi. Picha/ Margaret Maina

Mara nyingi tunaamka mapema kuwahi kazini au shuleni, tukisahau kuhusu staftahi. Labda watu wengi hawafahamu umuhimu wa chakula hiki kwani baada ya yote, bado kuna chakula cha mchana na chakula cha jioni.

Zipo faida nyingi za chakula hiki. Kiamshakinywa sahihi ni muhimu sana. Wakati huo huo, inatakiwa kufahamika kwamba vyakula vyote vyenye afya vinapaswa kuliwa asubuhi, ili tuweze kuwa na afya njema na nguvu ya kufanya kazi zetu za kila siku.

Ni bora kutilia maanani maoni ya wale wanaoita kifunguakinywa ‘msingi wa uzuri na afya’ na kula vyakula ambavyo vinafaa mwilini.

  • kiamshakinywa, huamsha kazi ya viongo na mifumo yote na kuongeza ufanisi wa shughuli zetu, haijalishi tunafanya nini;
  • husaidia kudhibiti uzani katika kiwango cha kawaida na kupunguza njaa;
  • hupunguza hisia za uchovu na usingizi kwa sababu ya kuongezeka kwa sukari yenye kuleta nguvu;
  • huimarisha uhusiano ndani ya familia kwani chakula cha asubuhi huleta pamoja wazazi, watoto na jamaa

Unaweza kuwa hapo na juisi ya machungwa au ya matunda mengineyo.

Juisi. Picha/ Margaret Maina

Unapoamua kunywa kahawa bila sukari na krimu, bila shaka italetea mwili faida.

Chai

Jumuisha chai ya kijani (green tea) au hibiscus katika kiamshakinywa chako.

Bidhaa za maziwa

Hizi ziwe ni sehemu ya staftahi kwa sababu husaidia kuanzisha michakato ya metaboli mwilini.

Kwa ukweli, kiamshakinywa chenye afya kweli haziwezi kuwa na mtindi au maziwa tu. Jaribu kuchanganya bidhaa za maziwa na sahani zingine (kwa mfano, uji.

Kakao

Hili zao la mkakao lina Vitamini, protini, na madini mengineyo muhimu kwa afya ya binadamu.