Makala

SIHA NA LISHE: Vifahamu vyakula vinavyoimarisha kinga mwilini

July 19th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

AFYA ya binadamu ni muhimu.

Ukiwa mwenye afya nzuri bila shaka utaweza kufanya mambo yako bila tatizo lolote. Kuna vyakula kadhaa vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya mwili wako.

Maziwa mtindi au gururu (Yoghurt)

Maziwa haya hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe; na hupatikana kwa ladha mbalimbali.

Matunda

Katika mlo wako wowote, jitahidi usiache kula angalau tunda moja la aina yoyote.

Mtu asiyekula matunda huwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa akilinganishwa na mlaji wa matunda.

Vitunguu saumu

Hupatikana kwa urahisi sokoni.

Ingawa vitunguu saumu vimekuwa vikitumika sana kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali, vitunguu hivi ni muhimu kwa kinga ya binadamu.

Unaweza kuvitumia ama kwa kutafuna au kwa kutia kwa chakula wakati wa mapishi.

Uyoga

Uyoga ni aina mojawapo ya vyakula muhimu zaidi vinavyoimarisha afya. Hii ni kwa sababu huchangia kiasi kikubwa kuimarisha seli nyeupe za damu zinazofanya kazi ya kupambana na magonjwa mbalimbali!

Viazi vitamu

Kwa kinga kamili ya mwilini, tunahitaji Vitamini A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu.

Karoti

Karoti zina vitamini kwa wingi.

Watu wengi wanatumia karoti kama kiungo kwenye chakula. Baadhi hutafuna karoti ikiwa mbichi.

Samaki

Husaidia seli nyeupe kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa na kadhalika.

Tikitimaji

Tunda hili ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilini, madini ya chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu.