SIHA NA USAFI: Jinsi ya kuondoa vipele puani (whiteheads)
Na MARGARET MAINA
HIVYO vitu vyeupe vilivyomo puani ni ngozi zilizokufa “dead skins” ambazo zikikutana na hewa zinasababisha upele (whiteheads).
Vipele hivyo ni aina ya chunusi na huwatokea zaidi watu wenye ngozi za mafuta, wanawake kwa wanaume, wazee kwa vijana.
Unaweza kuviondoa kwa kutumia facial cleansers na oil free moisturiser.
Osha uso mara mbili kwa siku na maji ya ufufutende.
Baada ya kuosha fanya kama unapigapiga taulo usoni “pat dry” usisugue. Hii ni njia inayopunguza uchafu na mafuta kujijenga kwenye mashimo ngozini.
Tumia Face cleanser ambayo itaondoa uchafu na seli zilizokufa kwenye ngozi.
Bidhaa za vipodozi vyenye viambata kama alpha-hydorxyl acid, salicylic acid au benzoyl-peroxide ni nzuri kwa kuondoa hivyo vitu.
Ulizia bidhaa hizo kwenye maduka ya vipodozi vya haiba na vya kuaminika na bila shaka utapata.
Steaming ni njia nzuri ya kuondoa vipele hivyo. Unachotakiwa kufanya ni kuchemsha maji kisha uyamimine kwenye bakuli. Acha ule mvuke ukupige usoni kwa muda wa robo saa. Hii ni njia nzuri ya kufungua tundu au vinyweleo kwenye ngozi ambapo inakuwa rahisi kuondoa uchafu kwenye ngozi.
Tumia skrabu kulingana na ngozi yako. Hii inaondoa ngozi iliyokufa na kusafisha ngozi.
Ukitoka kuoga, tumia vidole vyako viwili kusugua taratibu eneo la pua ,itaondoa ngozi zote zilizokauka.
Epuka kujishika eneo hilo wakati wote kwa sababu vijidudu vilivyopo kwenye mikono vinasababisha hali hiyo kuendelea au kuongezeka.
Kuna njia zingine pia ambazo mtu anaweza kutumia nyumbani kuondoa hivyo vipele.
Aloe vera
Aloe vera inaua vijidudu kwa kawaida na ina anti-oxidants.
Changanya matone matatu ya juisi ya limau na jeli ya Aloe vera. Weka kwenye uso, kisha sugua taratibu kwa robo saa. Baadaye safisha uso kwa kutumia maji moto.
Nyanya
Tengeneza juisi ya nyanya, chukua hii juisi na upake usoni mpaka ikauke. Kisha osha uso kwa maji fufutnde.
Asali
Pasha moto asali. Ikiwa na joto la kiasi – sio la kuunguza – paka usoni na usugue taratibu kwenye eneo la pua kwa dakika 10 halafu uache ikauke. Osha uso inapokauka.
Skrabu ya sukari
Saga sukari kisha changanya na juisi ya limau, weka kwenye eneo la pua na usugue taratibu. Baada ya dakika 20 osha.
Mayai
Mayai yana omega-3 fatty acids nyingi, vitamini na madini ambayo husaidia ngozi. Chukua kiini cha yai weka kwenye uso,ukishakauka osha uso wako na maji fufutende.