Trump anaanza ziara yake nchini Uingereza
RAIS wa Amerika, Donald Trump leo (Septemba 17,2025) ameanzisha ziara yake ya pili ya kitaifa nchini Uingereza ambayo watawala mjini London wanatumai itasaidia kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.
Trump na mkewe walikaribishwa na Mfalme Charles III kwenye kasri la Windsor kwa halfa ya fahari iliyojumuisha heshima ya gwaride la kijeshi.
Kwa desturi, Uingereza huwakaribisha viongozi wa kigeni kufanya ziara moja pekee ya kitaifa na Trump alipata heshima hiyo mwaka 2019 alipoalikwa kuitembelea Uingereza na Malkia Elizabeth II.
Hata hivyo ziara hii nyingine ambayo si ya kawaida inazingatiwa kuwa sehemu ya mkakati wa Uingereza wa kumweka karibu kiongozi huyo anayejulikana kwa sera zisizotabirika.