• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Mbinu ya mawasiliano (Communicative Language Approach)

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Mbinu ya mawasiliano (Communicative Language Approach)

Na MARY WANGARI

MKABALA huu unasisitiza maingiliano na maathiriano baina ya mwalimu, mwanafunzi pamoja na jamii.

Wataalamu wanaopigia debe nadharia hii wanasizitiza kwamba kujifunza lugha ni kujifunza kuwasiliana.

Aidha, wanasema kwamba kujua lugha kwa hakika sio kujua kanuni za lugha ile bali ni kujua namna ya kuwasiliana na watu wa jamii ile kwa kuzingatia mikitadha mbalimbali ambamo lugha hiyo inatumika.

Nadharia hii imeshaididiwa na wataalam wengi akiwamo Noamy Chomsky. Hii ndiyo nadharia mwafaka katika matumizi yanayohusu kujifunza lugha.

Viwango vya wanafunzi

Dhana hii inamaanisha uwezo alio nao mtu wa kutumia lugha fulani.

Viwango hivi viliwekwa na shirika lisilokuwa la kibiashara wala kiserikali linalofahamika kama Interagency Language Roundtable (ILRT).

Kwa mujibu wa shirika hili wanagenzi wa lugha wameainishwa katika viwango vitatu ambavyo ni:

Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw. DAMSA); Beginners Level

Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI); Intermediate Level

Wanafunzi wa daraja la juu (DAJUU); Advanced Level

Aidha, wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw. DAMSA) Beginners Level, wamegawanywa katika vitengo vifuatavyo:

0-® Katika kiwango hiki mwanafunzi hawezi kabisa kuzungumza lugh

Kiwango cha +0-® mwanafunzi amekaririshwa tu mahitaji muhimu akibadilishiwa tu basi anapotea mweleleo.

Kiwango cha  1-®  mwanafunzi anaweza kustahimili mazungumzo ya ana kwa ana ila hawezi kuanzisha mazungumzo

Kiwango cha +1-® mwanafunzi anaweza kuanzisha mazungumzo yeye mwenyewe, hata hivyo ni kwa ajili ya kukidhi matarajio yake

Sifa za wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI) Intermediate Level

Daraja la 2-lugha si kamilifu lakini mwanafunzi anaeleweka kwa urahisi

Kiwango cha 3 mwanafunzi anaweza kuzungumza lugha kwa muundo sahihi, ana msamiati wa mazingira fulani fulani tu ili kukidhi mahitaji ya kitaaluma

Anaweza kukidhi mahitaji ya kitaaluma

2+® Lugha yake si kamilifu lakini anaweza kueleweka kwa urahisi

3®  Mwanafunzi ana uwezo wa kuzungumza lugha kwa usahihi, ana msamiati toshelevu kwa mazingira fulani fulani tu.

 

[email protected]

 

Marejeo

Todd, L. (1987). An Introduction to Linguistics. Essex: Longman Group Limited.

TUKI (1990). Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Yule, G. (2010). The Study of Language (4th ed.). Cambridge: Cambridge University Press.

You can share this post!

Raga ya Wanawake: Kocha Felix Oloo akitaja kikosi...

Wandani wa Ruto wataka wafafanuliwe maana ya demokrasia...

adminleo