Makala

ULIMBWENDE: Jinsi ya kutunza ngozi zenye mafuta

April 10th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Sababu ya ngozi kuwa na mafuta hutokana na tezi za ‘sebaceous’ na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango ambacho kinatakiwa.

Lakini licha ya tezi hizo aina ya sebaceous kuzalisha kiwango cha mafuta kwa wingi, zipo pia sababu nyingine ambazo zinafanya ngozi kuwa na mafuta ambazo ni kama ifuatavyo.

• Kurithi
• Lishe
• Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini
• Ujauzito
• Baadhi ya vipodozi
• Mabadiliko ya hali ya hewa hasa joto

Madhara ambayo yanatokana na ngozi yenye mafuta ni kwamba, ngozi huweza kutengeneza tabaka lisiloisha, vipele pamoja na chunusi kwa muda mrefu.

Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta ni kama ifuatavyo:

Kuosha uso vyema kwa kutumia maji moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta. Ni muhimu kusafisha uso mara mbili au mara tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.

Ni muhimu kuepuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi ya mtumiaji ipoteze maji au kukauka. Vinaweza kusababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kusababisha kutokea kwa chunusi ambazo zitaufanya mwili kuwa na mafuta.

Chagua kile unachosafishia uso wako kwa makini. Epuka kutumia mafuta mazito au vifaa vigumu wakati wa kuosha uso wako.

Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na dawa. Unaweza kutumia losheni ya kuua bakteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia losheni au michanganyiko yenye alkoholi au pombe.

Pia ni vyema kutumia mafuta ambayo yametengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.

Endapo utayazingatia hayo mwili wako utakwenda kuwa katika hali ya ubora zaidi, na kufurahia ngozi isiyo na kasor