Makala

VIDUBWASHA: Beba mkalimani wako mfukoni

May 28th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na LEONARD ONYANGO

SASA inawezekana kuzungumza na mtu asiyefahamu lugha unayoiongea bila kuwa na mkalimani.

Kifaa cha Pocketalk kimeondoa usumbufu wa kutafuta mkalimani kwani kinaweza kutafsiri zaidi ya lugha 70.

Kwa mfano, ikiwa wewe unatumia lugha ya Kiingereza na mtu unayewasiliana naye hafahamu lugha hiyo na badala yake anaongea Kifaransa, mnaweza kuelewana kwa kutumia kifaa hiki.

Kifaa hiki kinatafsri lugha maarufu zinazotumiwa katika ulingo wa kimataifa. Haijulikani ikiwa siku moja kifaa hicho kitatufaa hapa nchini kwa kusaidia Mmeru kuzungumza lugha ya Kimeru na Mjaluo bila kuwepo kwa mkalimani.

Iwapo kifaa hicho kitafika humu nchini, basi kitakuwa ni afueni kwa wanasiasa kwani mwanasiasa kutoka Nyanza, kwa mfano, ataweza kuhutubia mkutano wa kisiasa huko Turkana kwa kutumia lugha ya Dholuo na kitatafsiria umati.