• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
VIDUBWASHA: Hupunguzia wajawazito hatari (MobiUS SP1 System)

VIDUBWASHA: Hupunguzia wajawazito hatari (MobiUS SP1 System)

Na LEONARD ONYANGO

KULINGANA na ripoti ya Shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Kenya ni miongoni mwa mataifa hatari zaidi kwa akina mama kujifungulia.

Hii inatokana na uhaba wa wataalamu au madaktari wa kusaidia akina mama kujifungua, uhaba wa hospitali haswa katika maeneo yaliyo mbali na miji na ukosefu wa vifaa vya kutosha.

Kwa mujibu wa UNFPA, wanawake zaidi ya 400 kati ya 100,000 hufariki kila mwaka kutokana na matatizo yanayohusiana na uzazi.

Sasa kifaa kipya cha MobiUS SP1 System huenda kikasaidia kupunguza maafa hayo iwapo kitakumbatiwa na maafisa wa afya humu nchini.

Kifaa hicho kinachounganishwa na simu kinatumika kupima akina mama wajawazito hata katika maeneo ambapo hakuna hospitali.

Kinatumika kupima afya ya mtoto aliye tumboni kwa kufuatilia mapigo ya moyo kati ya mambo mengineyo.

Aidha hunasa picha ya mtoto aliye tumboni na matokeo yanaweza kutumwa kwa mtu mwingine kwa kutumia mtandao.

You can share this post!

Kiberiti hiki ni adui ya sigara

Polisi wakamata washukiwa watatu wa genge la uvamizi Bamburi

adminleo