Makala

VIDUBWASHA: Hutahitaji kadi sakima (Samsung Galaxy M40)

June 4th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na LEONARD ONYANGO

KAMPUNI ya Samsung ya Korea Kusini inaonekana kuonyesha ubabe wake katika soko la simu za mkononi ili kukabiliana na ushindani mkali kutoka kwa kampuni za China kama vile Oppo na Huawei.

Miezi michache baada ya kuzindua simu tatu za toleo la Galaxy M10, Galaxy M20 na Galaxy M30, Jumapili, Samsung ilizindua Galaxy 40 ambayo huenda ikawa kivutio kwa wapenzi wa kamera zinazonasa picha na video za ubora wa hali ya juu.

Kamera ya nyuma ina megapikzeli 48MP.

Inahifadhi data ya ukubwa wa 128 GB bila kuongezewa kadi sakima (memory card).

Simu hii ina kitundu hapo juu ambacho kimezua shaka kubwa miongoni mwa watumiaji.