Makala

VIDUBWASHA: Huua bakteria kwenye maji (SteriPEN)

August 6th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na LEONARD ONYANGO

WATAALAMU wa afya wanasema kuwa maji machafu huwa na mamilioni ya bakteria ambao ni hatari kwa afya.

Maji huwa na aina mbalimbali za bakteria ambazo hujumuisha: ‘Escherichia Coli’, ‘Campylobacter Jejuni’, ‘Hepatitis A’, ‘Giardia Lamblia’ na ‘Salmonella’.

‘Escherichia Coli’ husababisha tumbo kuuma, kutapika na kuhara unapoinywa kwenye maji na dalili zake huonekana ndani ya siku nane.

‘Campylobacter Jejuni’ husababisha maumivu, joto mwilini na dalili zake hujitokeza kati ya siku mbili na 10 tangu kuingia mwilini.

Dalili za ‘Hepatitis A’ ni mkojo unaoonekana mchafu, maumivu ya tumbo na uchovu na hujitokeza baada ya siku 28 baada ya kunywa maji machafu.

‘Giardia Lamblia’ husababisha gesi tumboni na dalili zake hujitokeza baada ya wiki mbili.

‘Salmonella’ ni bakteria wanaosababisha maumivu ya kichwa, tumbo na husababishia mwathiriwa baridi na dalili zake hujitokeza ndani ya siku tatu.

Kifaa cha SteriPEN, hata hivyo, kinakuondolea wasiwasi wa kunywa maji ukiwa na hofu ya kupata bakteria.

Kinaua asilimia 99.9 ya bakteria katika maji ya kunywa kwa kutumia miale ya UV.

Kinatibu maji ndani ya sekunde 45.