VIDUBWASHA: Simu ya kwanza kutumia masafa ya 5G
Na LEONARD ONYANGO
KAMPUNI ya Oppo ya nchini China imekuwa ya kwanza kuingiza sokoni simu zake zinazotumia masafa ya 5G.
Simu zinazotumia masafa ya 5G zinasakura kwa kasi ya juu mtandaoni ikilinganishwa na simu za sasa zinazotumia 4G, 3G au 2G.
Nchini Kenya, mtandao wa 4G bado haujafikia kaunti nyingi hivyo simu ya 5G huenda isikufae humu nchini.
Simu ya Oppo Reno ilizinduliwa rasmi mnamo Aprili 10 nchini China kisha ikazinduliwa Uswizi.
Mataifa mengi kama vile Amerika na Uingereza yamekuwa yakichelea mtandao wa 5G kutumiwa kutokana na hofu kwamba huenda wadukuzi wakautumia kuiba taarifa za kisiri za serikali.
Naibu Rais wa kampuni ya Oppo, Shen Yiren, alisema kuwa simu hiyo ya aina yake itasambazwa katika masoko mbalimbali kufikia mwishoni mwa mwaka 2019.
Ina uwezo wa kuhifadhi data ya 256GB bila kuwekewa kadi sakima(memory card). Ina kamera tatu mbele na moja ya selfie.