VINYWAJI: Jinsi ya kutayarisha sharubati ya karakara na tini 'beetroot'
Na MISHI GONGO
KINYWAJI hiki ni kizuri kwa afya ya binadamu kwa sababu tunda la tini – beetroot – husaidia kuongeza damu mwilini.
Idadi ya wanywaji: 4
Vitu vinavyohitajika
- beetroot 1/2
- karakara 4
- karoti kubwa 2
- sukari nusu kikombe
Namna ya kutayarisha
Anza kwa kuosha matunda yako kisha tayarisha upate juisi.
Katakata beetroot na karoti vipandeĀ vidogovidogo kisha weka ndani ya jagi la kusagia (blenda).
Kata karakara, ongeza juisi yake ndani ya jagi la kusagia.
Ongeza sukari na iliki tembe tatu ndani ya jagi.
Ongeza maji glasi nne ndani ya mchanganyiko kisha saga hadi mchanganyiko ulainike.
Chukua chombo safi kisha chuja mchanganyiko wako kwa kichujio kutoa mathapu.
Unaweza kuweka katika jokofu ikawa baridi au unaweza kunywa vivyo hivyo.