• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 3:36 PM
Vyakula vya kusaidia ubongo na kumbukumbu

Vyakula vya kusaidia ubongo na kumbukumbu

Na MARGARET MAINA

[email protected]

AFYA ya akili inategemea mfumo mzuri wa uimarishwaji wa afya ya ubongo wako.

Kuna vyakula vingi na matunda yanayohusiana na kuimarisha afya ya ubongo.

Mafuta ya samaki

Samaki ana mafuta ambayo ni muhimu katika mwili.

Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili.

Pilipili

Pilipili kali nayo huwa ni chakula muhimu kwa ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamini C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo.

Mbegu za maboga

Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuimarisha uwezo wa kumbukumbu. Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, kula kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, unaweza kuzisaga na kupata unga ukawa unautumia kwa kunywea kwenye chai au kulamba.

Nyanya

Nyanya. Picha/ Margaret Maina

Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.

Brokoli

Brokoli. Picha/ Margaret Maina

Brokoli ni mboga ambayo ina faida sana kwenye ubongo kwani ina vitamini K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamini K inahusika na utendaji kazi mzuri wa ubongo.

Karanga

Aina zote za karanga zina Vitamini E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

Mayai

Mayai ya kuku, yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza, kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.

You can share this post!

Wanawake zaidi ya 10,000 Mukuru wapigwa jeki kwa kupewa...

PSG kumsajili Dele Alli baada ya kubanduka Spurs mnamo...