• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 6:55 PM
Beki Arthur Melo kuelekea Juventus huku Miralem Pjanic akitarajiwa kutua Camp Nou

Beki Arthur Melo kuelekea Juventus huku Miralem Pjanic akitarajiwa kutua Camp Nou

Na CHRIS ADUNGO

JUVENTUS wameafikiana na Barcelona kuhusu kumsajili kiungo Arthur Melo mwishoni mwa msimu huu.

Nyota huyo mzawa wa Brazil atabanduka rasmi uwanjani Camp Nou na kutua Juventus kwa kima cha Sh9.2 bilioni huku kiasi hicho cha fedha kikitarajiwa kuongezeka kwa Sh1.2 bilioni zaidi iwapo Juventus watawazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mwishoni mwa msimu huu.

Arthur, 23, aliingia katika sajili rasmi ya Barcelona baada ya kukatiza uhusiano wake na Gremio ya Brazil kwa mkataba wa miaka sita mnamo 2018. Tangu wakati huo, sogora huyo amewajibikia Barcelona katika jumla ya michuano 72.

Kukamilika kwa uhamisho wa Arthur hadi Juventus kutamshuhudia pia kiungo mzawa wa Bosnia, Miralem Pjanic, 30, wa Juventus akielekea Barcelona kwa mkataba wa miaka mitano.

Pjanic ambaye amechezea Juventus jumla ya mechi 214 tangu 2016, atajiunga na Barcelona kwa kima cha Sh7.7 bilioni huku kiasi hicho cha fedha kikiongezeka kwa Sh644 milioni iwapo Barcelona pia watafuzu kwa kivumbi cha UEFA muhula ujao.

Kufikia sasa, Juventus kwa sasa wanaselelea kileleni mwa jedwali la Serie A kwa alama nne zaidi kuliko nambari mbili Lazio kadri wanavyofukuzia kutia kapuni taji lao la tisa mfululizo.

You can share this post!

Straika Mitrovic wa Fulham apigwa marufuku mechi tatu kwa...

AFUENI: Wachezaji wawili wa raga kusimama kizimbani tena

adminleo