• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Juventus katika hatari ya kukosa UEFA msimu ujao

Juventus katika hatari ya kukosa UEFA msimu ujao

Na MASHIRIKA

AC Milan waliwapeteta Juventus 3-0 katika mchuano wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A) uliochezewa jijini Turin mnamo Mei 9, 2021.

Matokeo hayo yalisaza Juventus katika hatari ya kukosa kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao.

Zikisalia mechi tatu pekee kwa kampeni za Serie A msimu huu kutamatika rasmi, Juventus kwa sasa wanashikilia nafasi ya tano jedwalini kwa alama 69, moja nyuma ya Napoli wanaofunga orodha ya nne-bora.

AC Milan wanakamata nafasi ya tatu kwa alama 72 sawa na Atalanta wanaoshikilia nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Inter Milan wanaojivuni pointi 85.

Brahim Diaz alifunguliwa AC Milan ukurasa wa mabao mwishoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya Ante Rebic kuongeza la pili kunako dakika ya 78. Beki Fikayo Tomori anayechezea AC Milan kwa mkopo kutoka Chelsea ndiye alizamisha kabisa chombo cha Juventus kwa kupachika wavuni goli la tatu katika dakika ya 82.

Juventus kwa sasa wako nje ya orodha ya nne-bora jedwalini huku zikisalia mechi tatu zaidi msimu huu, ikiwemo ile itakayowakutanisha na Inter Milan ya kocha Antonio Conte. Inter walitawazwa mabingwa wa Serie A muhula huu kwa mara ya kwanza tangu 2009-10.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Rennes yadidimiza matumaini finyu ya PSG kuhifadhi taji la...

West Brom washuka ngazi kutoka EPL baada ya kupepetwa na...