• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 1:33 PM
Corona ilivyobadilisha maisha ya wanasoka mashinani

Corona ilivyobadilisha maisha ya wanasoka mashinani

Na JOHN KIMWERE

JANGA la virusi hatari vya corona kamwe halitawahi kusaulika miongoni mwa wadau wa soka baada ya kusababisha shughuli za michezo kusitishwa kote duniani.

Dah! Si soka, si riadha, si voliboli, si mpira wa kikapu, si handiboli, si voliboli, si karate, si Tae Kwo Ndo pia mashindano ya magari lilichangia kupigwa stopu.

Kikubwa zaidi pia mashindano ya Olimpiki yangeandaliwa nchini Japan mwezi Julai mwaka huu nayo pia yalisitishwa na kuhairishwa ambapo sasa yamepangwa kuandaliwa mwaka ujao.

Mkurupuko huo unaendelea kuzima shughuli za michezo kote barani Afrika hakika umepasua vichwa vya wadau wengi tu. Kadhalika janga hili limechanganya makocha na wamiliki wa klabu zilizokuwa zinashiriki mechi za vipute vya juu bila kusahau michezo ya mashinani.

Timu ya South B pia inayoshiriki kipute cha NWRL.

MASWALI KIBAO

Ni janga lililochangia rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Nick Mwendwa kutangaza kumaliza ligi tatu za mchezo huo Ligi Kuu ya KPL, Betika Supa Ligi ya Taifa (BNSL) na Ligi ya Taifa Daraja la Pili.

Kwa vipute vya chini hali hali ni ngori buda hakika hakieleweki. Kwa ngarambe ya Nairobi West Regional League (NWRL) washiriki wanajiuliza maswali kibao na kutoa maoni mbali mbali kwa kuzingatia muda unakwenda kama moshi hasa wa kumaliza kampeni za kipute hicho.

Kocha wa Riara University, Owen Makokha amesema kwamba viongozi wa tawi hilo wana wakati mgumu hasa jinsi watakavyoamua hatima ya kipute hicho.

”Kampeni zetu zilisitishwa wakati hatukuwa tumepiga kazi kubwa maana hakuna timu iliyokuwa imekamilisha mechi zote za mkumbo wa kwanza,” anasema na kuongeza kuwa suala hilo ndilo linalochangia viongozi hao kuwaza na kuwazua jinsi vipute wanavyosimamia.

Kenya School of Government (KSG) maarufu Ogopa FC inayoshiriki kipute cha NWRL.

KUPIGA SOGA

Anadokeza kwamba jambo nzuri viongozi wa tawi hilo wanalostahili kufanya ni kufute cha muhula huu na kuweka mikakati ya kuanza kwa michuano ya msimu ujao.

Kocha huyo akipiga soga na Taifa Leo Dijitali mwandishi wetu alisema kuwa endapo hawatachukua hatua hiyo bila shaka hawatakuwa wanatendea haki kwa timu za ngarambe ya msimu huu.

Kando na hayo kwa upande wa kikosi chake alisema licha ya kwamba mkurupuko wa corona ulichangia shule kwa jumla taasisi za masomo zote kufungwa.

Wachezaji wa Silver Bullets washiriki wa NWRL.

MWEZI SEPTEMBA

”Kwa muda huu wachezaji wangu hawapo karibu ambapo hata mechi za ligi zikirejelewa leo binfasi nitakosa wachezaji wangu,” alisema na kuongeza kwa maoni anadhani kwa jinsi hali inavyoendelea endapo mambo yatakaa vizuri pengine vyuo vitafunguliwa mwezi Agosti ama Septemba mwaka huu.

Muda mechi hizo zilipositishwa Riara University ilikuwa imekaa vibaya kwenye jedwali la kipute hicho.

You can share this post!

Corona imesaidia kukabiliana na magonjwa mengine –...

Tutawakabili wapinzani vilivyo – Mbotela Kamaliza

adminleo