• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
FATAKI ZA FA: Manchester City mavizioni jicho sasa likiwa kwa FA Cup

FATAKI ZA FA: Manchester City mavizioni jicho sasa likiwa kwa FA Cup

Na MASHIRIKA

MANCHESTER, Uingereza

MANCHESTER City wanatarajiwa kuendeleza ukatili wao watakapokutana na Sheffield Wednesday leo Jumatano usiku ugenini katika gozi la FA Cup kuania nafasi ya kufuzu kwa robo-fainali ya michuano hiyo ya kitaifa.

Wenyeji wataingia uwanjani baada ya majuzi kuchapwa mabao 3-1 na Derby County katika pambano la Daraja la Kwanza mwishoni mwa wiki.

Lakini City watateremka uwanjani wakijivunia ubingwa wa Carabao (League Cup) kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuilaza Aston Villa 2-1 fainalini.

Kwa sasa City wanaendelea kushikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Vijana hao wa kocha Pep Guardiola walichapa Watford mabao 6-0 katika fainali ya FC Cup msimu uliopita, mbali na kuhifadhi ubingwa wa EPL.

Lakini licha ya kushindwa kuvuma kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita, Manchester City wameshinda mechi nne mfululizo katika mashindano tofauti, ukiwemo ushindi wa majuzi wa mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa, ugani Wembley.

Marufuku yao ya miaka miwili kutoka kwa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) haionekani kuvuruga mipango ya Guardiola, kwani ni majuzi tu walipoikung’uta Real Madrid 2-1 ugani Bernabeu na kurejesha matumaini ya mashabiki wa Etihad ambao walikuwa na wasiwasi kuhusu mwenendo wa timu hiyo.

Tayari Guardiola amekiri kwamba kazi yake pale Etihad haiwezi kukamilika bila ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya.

City ilisonga mbele baada ya kuzibandua Port Vale na Fulham na kutinga raundi ya tano, lakini wakati huu inakutana na timu ambayo hawajawahi kuishinda kwa muda mrefu.

Ni takbani miaka 85 tangu Wednesday washinde ubingwa wa FA Cup, baada ya kuibwaga West Bromwich Albion 4-2 msimu wa 1934-35.

Mabingwa hao mara tatau wa taji hilo walitinga fainali kwa mara ya mwisho mnamo 1993, dhidi ya Arsenal katika mechi iliyomalizika kwa 1-1 kabla ya kushindwa 2-1 katika marudiano, baada ya muda wa ziada kumalizika zikiwa hivyo – 1-1.

Mechi nyingine za kuwania nafasi ya kufuzu kwa robo-fainali ni Tottenahm Hotspur na Norwich City, Leicester City na Birmingham.

You can share this post!

SGR: Mizigo imeleta faida, abiria wamepungua – Ripoti

Meno ya makinda wa Arsenal yapewa sifa

adminleo