• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Kikosi cha Equatorial Guinea kilinifurahisha nikakubali kuwa kocha – Migne

Kikosi cha Equatorial Guinea kilinifurahisha nikakubali kuwa kocha – Migne

Na JOHN ASHIHUNDU

ALIYEKUWA kocha wa Harambee Stars, Sebastien Migne ameeleza kilichomshawishi akubali kuwa kocha wa Equatorial Guinea.

Mfaransa huyo aliwaambia waandishi habari kwamba aliikubali kazi hiyo baada ya kufurahishwa na kikosi kizima.

“Nilipokuwa kocha wa Harambee Stars ya Kenya, niligundua ubora wa kikosi cha Equatorial Guinea ambacho kilinifurahisha kwa kuwa na wachezaji wengi wazuri. Niliamini wakati mmoja nitapata nafasi ya kuinoa timu hii. Mara tu nilipoitwa, nikakubali haraka,” alisema.

Migne aliyekuwa chini ya mkongwe Claude Le Roy ambaye amekuwa kwa muda wa miaka tisa alisema mtihani wake wa kwanza ni kuhakikisha timu hiyo imefuzu kwa fainali za Qatar 2022 baada ya mechi za mchujo ambazo pia zinajumuisha na Tunisia, Zambia na Mauritania.

“Bila shaka ni kundi gumu, lakini tutapigana vikali hadi dakika ya mwisho. Tumejifunza mengi katika mechi za awali za kimataifa. Nchi hii haijawahi kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia. Lakini kuna matumaini makubwa, huku tukitarajia mambo mengi mazuri siku za usoni,” alisisitiza.

You can share this post!

Corona yakosesha kazi Wakenya zaidi ya 300,000

Uwanja wa San Siro unaotumiwa na AC Milan na Inter Milan...

adminleo