• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 5:46 PM
Kwa mara ya kwanza, uwezo wa Arsenal kutwaa ubingwa wa ligi umepita wa Liverpool – Ubashiri

Kwa mara ya kwanza, uwezo wa Arsenal kutwaa ubingwa wa ligi umepita wa Liverpool – Ubashiri

Na GEOFFREY ANENE

UWEZO wa Arsenal kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu wa 2023-2024 umepita wa Liverpool katika vita vya farasi watatu vinavyohusisha pia Manchester City.

Kwa mujibu wa ubashiri mpya wa kompyuta maalum ya Opta, asilimia ya Arsenal kushinda ligi hiyo ya klabu 20 imeongezeka kutoka 21.4 hadi 30.3 baada ya kulipua Brighton 3-0.

Uwezo wa Liverpool ya kocha Jurgen Klopp umepungua kwa asilimia 15.9 kutoka 45.0 hadi 29.1 baada ya kutoka 2-2 dhidi ya mahasimu wa tangu jadi Manchester United.

Mabingwa watetezi City wanaofukuzia taji la nne mfululizo, wana uwezo wa kutwaa ubingwa wa ligi wa asilimia 40.6 baada ya kuimarika kwa asilimia 7.0 kutoka 33.6 kufuatia ushindi wa 4-2 dhidi ya Crystal Palace.

Huku ligi hiyo ikiendelea kupamba moto na kusalia mechi saba kabla ya kutamatika, Opta pia inaamini kuwa timu itakayofanya makosa machache kutoka kwa orodha ya Arsenal (alama 71), Liverpool (71) na City (70) itakuwa na fursa nzuri ya kushinda ligi.

Mara ya mwisho Arsenal walishinda ligi ni msimu 2003-2004 nao Liverpool ni 2019-2020.

RATIBA YA EPL:

Aprili 13 –

Newcastle vs Tottenham (2.30pm), Brentford vs Sheffield

United (5.00pm), Manchester City vs Luton Town (5.00pm),

Nottingham Forest vs Wolves (5.00pm), Burnley vs Brighton

(5.00pm), Bournemouth vs Manchester United (7.30pm);

Aprili 14 –

Liverpool vs Crystal Palace (4.00pm), West Ham vs Fulham (4.00pm),

Arsenal vs Aston Villa (6.30pm); Aprili 15 – Chelsea vs Everton

(10.00pm).

  • Tags

You can share this post!

Nashuku mke wangu anamgawia bosi wake asali, nishauri

Raphael Varane kupigwa bei ya jioni na Man United

T L