Michezo

Liverpool yaelekea kufuzu 16-bora baada ya kupepeta masogora Genk

November 7th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MASHIRIKA

MERSEYSIDE, Uingereza

USHINDI wa 2-1 dhidi ya Genk umewaongezea Liverpool matumaini ya kufuzu kwa hatua ya 16 Bora katika michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya.

Vijana hao wa kocha Jurgen Klopp, wamepanda hadi nafasi ya kwanza jedwalini katika Kundi E kufuatia bao la ushindi la Alex Oxlade-Chamberlin, likiwa bao lake la nne katika mchi nne.

Lakini baada ya Napoli, walishindwa kuichapa Salzburg, Liverpool wanaweza kufuzu iwapo wataandikisha ushindi dhidi ya Napoli kwenye mechi yao ijayo.

Ni matokeo yanayoweza kupatikana ikikumbukwa kwamba vijana hao wa Klopp wamecheza mechi 24 za michuano hii nyumbani bila kushindwa, ingawa kocha huyo ameeleza wasiwasi wake kuhusu ratiba ngumu ya mwezi Disemba kabla ya kusafiri ugenini kucheza na Salzbury.

Liverpool ambao Jumapili watakutana na Manchester United, walitangulia kupata bao la kwanza kupitia kwa Georginio Wiljnaldum kabla ya Chamberlin kupachika wavuni la ushindi katika kipindi cha pili.

Juhudi za Genk kusawazisha bao hilo ziliambulia patupu kutokana na kazi nzuri ya kipa Alisson aliyeokoa makombora kadhaa kutoka kwa washambuliaji matata akiwemo mfungaji Mbwana Samatta, raia wa Tanzania.

Kocha Klopp alimpanga Chamberlin katika nafasi ya Roberto Firmino kushirikiana na Mohamed Salah na Divock Origi, mabadiliko ambayo yalichanganya kikosi cha Genk.