Orodha ya wanaowania tuzo za FIFA
Na GEOFFREY ANENE
MWANASOKA bora duniani wa mwaka 2018 atajulikana kutoka orodha ya Cristiano Ronaldo, Luka Modric na Mohammed Salah wakati Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) litakapotangaza mshindi wa tuzo hii ya kifahari jijini London nchini Uingereza mnamo Septemba 24, 2018.
Ronaldo anapigiwa upatu kutwaa taji hili. Mshambuliaji huyu kutoka Ureno amewahi kushinda tuzo hii mwaka 2008, 2013, 2014, 2016, 2017. Alimaliza katika nafasi ya pili mwaka 2009, 2011, 2012 na 2015 nyuma ya mvamizi matata wa Argentina Lionel Messi. Nafasi mbaya Ronaldo amewahi kumaliza katika tuzo hizi baada ya kuorodheshwa kama mwaniaji ni nambari tatu mwaka 2007 nyuma ya mshindi Kaka (Brazil) na Messi.
Kuna vitengo tisa katika tuzo hizi za kila mwaka za FIFA ambapo washindi watajulikana leo Jumatatu.
VITENGO NA WAWANIAJI
Mwanasoka bora wa mwaka duniani (mwanamume): Cristiano Ronaldo (Juventus/Real Madrid), Luka Modric (Real Madrid) ama Mohamed Salah (Liverpool)
Mwanasoka bora wa mwaka duniani (mwanamke): Ada Hegerberg (Lyon), Dzsenifer Maroszan (Lyon) ama Marta (Orlando Pride)
Kocha bora wa mwaka duniani: Didier Deschamps (Ufaransa), Zinedine Zidane (Real Madrid) ama Zlatko Dalic (Croatia)
Kipa bora wa mwaka duniani: Thibaut Courtois (Real Madrid/ Chelsea), Hugo Lloris (Tottenham) ama Kasper Schmeichel (Leicester City)
Bao safi (Fifa Puskas Award): Gareth Bale (Real Madrid), Denis Cheryshev (Urusi), Lazaros Christodoulopoulos (AEK Athens), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Giorgian de Arrascaeta (Cruzeiro), Riley McGree (Newcastle Jets), Lionel Messi (Argentina), Benjamin Pavard (Ufaransa), Ricardo Quaresma (Ureno), Mohamed Salah (Liverpool)
Tuzo ya nidhamu ya juu:
Shabiki wa mwaka: Sebastian Carrera (Puerto Montt), mashabiki wa Peru, Japan na Senegal
Wanasoka 11 bora (Fifa FIFPro World XI): Watachaguliwa kutoka kwa orodha ya wawaniaji 55. Orodha yenyewe hii hapa chini:
Makipa (5)
Gianluigi Buffon – Italia, Juventus/Paris Saint-Germain
Thibaut Courtois – Ubelgiji, Chelsea/Real Madrid
David De Gea – Uhispania, Manchester United
Keylor Navas – Costa Rica, Real Madrid
Marc-Andre ter Stegen – Ujerumani, Barcelona
Mabeki (20)
Jordi Alba – Uhispania, Barcelona
Dani Alves – Brazil, Paris Saint-Germain
Daniel Carvajal – Uhispania, Real Madrid
Giorgio Chiellini – Italia, Juventus
Virgil van Dijk – Uholanzi, Southampton/Liverpool
Diego Godin – Uruguay, Atletico Madrid
Mats Hummels – Ujerumani, Bayern Munich
Joshua Kimmich – Ujerumani, Bayern Munich
Dejan Lovren – Croatia, Liverpool
Marcelo – Brazil, Real Madrid
Yerry Mina – Colombia, Barcelona/Everton
Benjamin Pavard – Ufaransa, Stuttgart
Gerard Pique – Uhispania, Barcelona
Sergio Ramos – Uhispania, Real Madrid
Thiago Silva – Brazil, Paris Saint-Germain
Kieran Trippier – Uingereza, Tottenham Hotspur
Samuel Umtiti – Ufaransa, Barcelona
Raphael Varane – Ufaransa, Real Madrid
Sime Vrsaljko – Croatia, Atletico Madrid/Inter
Kyle Walker – Uingereza, Manchester City
Viungo (15)
Sergio Busquets – Uhispania, Barcelona
Casemiro – Brazil, Real Madrid
Philippe Coutinho – Brazil, Liverpool/Barcelona
Kevin De Bruyne – Ubelgiji, Manchester City
Eden Hazard – Ubelgiji, Chelsea
Andres Iniesta – Uhispania, Barcelona/Vissel Kobe
Isco – Uhispania, Real Madrid
N’Golo Kante – Ufaransa, Chelsea
Toni Kroos – Ujerumani, Real Madrid
Nemanja Matic – Serbia, Manchester United
Luka Modric – Croatia, Real Madrid
Paul Pogba – Ufaransa, Manchester United
Ivan Rakitic – Croatia, Barcelona
David Silva – Uhispania, Manchester City
Arturo Vidal – Chile, Bayern Munich/Barcelona
Washambuliaji (15)
Karim Benzema – Ufaransa, Real Madrid
Edinson Cavani – Uruguay, Paris Saint-Germain
Paulo Dybala – Argentina, Juventus
Antoine Griezmann – Ufaransa, Atletico Madrid
Harry Kane – Uingereza, Tottenham Hotspur
Robert Lewandowski – Poland, Bayern Munich
Romelu Lukaku – Ubelgiji, Manchester United
Mario Mandzukic – Croatia, Juventus
Sadio Mane – Senegal, Liverpool
Kylian Mbappe – Ufaransa, Paris Saint-Germain
Lionel Messi – Argentina, Barcelona
Neymar Junior – Brazil, Paris Saint-Germain
Cristiano Ronaldo – Ureno, Real Madrid/Juventus
Mohammed Salah – Misri, Liverpool
Luis Suarez – Uruguay, Barcelona