Ratiba ya SportPesa Shield baada ya timu 5 kujiondoa
Na GEOFFREY ANENE
KLABU za Mathare United, Chemelil Sugar, Zoo Kericho, Thika United na Nakumatt kutoka Ligi Kuu zimesusia mashindano ya soka ya Kombe la Ngao yanayofahamika sasa kama SportPesa Shield.
Sababu ya klabu hizi kutokuwa makini na kombe hili linalotumika kuchagua mwakilishi wa Kenya katika Kombe la Mashirikisho la Afrika (Confederations Cup) haijabainika wazi.
Hata hivyo, burudani hili linatarajiwa kuwa moto baada ya klabu zingine 13 kutoka Ligi Kuu kutoa ithibati ya kushiriki.
Klabu hizo ni AFC Leopards (mabingwa watetezi), Bandari, Tusker, Posta Rangers, Kakamega Homeboyz, Ulinzi Stars, Nzoia Sugar, Vihiga United, SoNy Sugar, Wazito, Kariobangi Sharks, Gor Mahia na Sofapaka.
Mshindi Kombe la Ngao huzoa Sh2 milioni na kuingia Confederations Cup. Leopards inatetea taji ililonyakua baada ya kulipua Kariobangi Sharks 2-0.
Ratiba (SportPesa Shield):
Mwatate United vs Fortune Sacco
Ushuru FC vs Nunguni FC
Bandari FC vs Berlin FC (Garissa)
Tusker FC vs Taita Taveta FC
Leysa FC vs Emmausians (Tana River)
KCB FC vs Nanyuki All Stars
Sofapaka FC vs Re-Union
Equity Bank FC vs Baba Dogo United
Naivas FC vs Friend Zone FC
Zetech University vs Tandaza FC
Gor Mahia FC vs SS Assad (Mombasa)
Savannah Cement FC vs KenPoly FC
Kariobangi Sharks FC vs Nanyuki Youth
Wazito FC vs Nairobi Water FC
Talanta FC vs Ligi Ndogo FC
Modern Coast FC vs Balaji FC
SoNy Sugar FC vs Rain Forest
AFC Leopards vs Shabana FC
GFE 105 vs VegPro FC
Vihiga United FC vs Nyamira All Stars
Kisumu All Stars vs MKU Nakuru
Nakuru All Stars vs River Plate
Kenya Police vs Nakuru West Combined
Nzoia Sugar FC vs Dero FC
Ulinzi Stars FC vs Transmilan FC
Kakamega Homeboyz FC vs ASEC FC
Western Stima FC vs Egerton University
Bidco FC vs Kabras United
Posta Rangers FC vs Transmara Sugar FC
Raiply vs Kisumu Hot Stars
Timsales vs Bungoma Super Stars
Eldoret Youth vs Transfoc