Habari Mseto

Polisi akataa hongo ya Sh80,000 kuachilia mshukiwa

March 2nd, 2024 1 min read

NA WINNIE ONYANDO

TUME ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imepongeza hatua ya mkuu wa polisi (OCS) wa kituo cha Polisi cha Archers katika Kaunti ya Samburu, Andrew Nyabicha ya kukataa kupokea hongo ya Sh80,000.

Hii ni baada ya watu watatu kujaribu kumhonga ili akubali kumuachilia mshukiwa wa wizi Mohamed Musdaf Mahamad.

Washukiwa hao walitambuliwa kama George Guyo, askari wa gereza kutoka Isiolo Hassan Sheikh Mohamed, na Mohamed Maalim Abass.

Baada ya kubaini nia yao, Bw Nyabicha aliripoti mpango huo wa ufisadi kwa EACC.

Msemaji wa EACC Eric Ngumbi, alimsifu Bw Nyabicha huku akiwarai maafisa wengine kuiga mfano wake.

“EACC inampongeza mkuu huyo wa kituo kwa hatua aliyochukua. Maafisa wengine pia wanafaa kuiga mfano huo ili tuweze kukabili ufisadi nchini,” akasema Bw Ngumbi.