Mbunge wa Lari na maafisa wa CDF wakamatwa
Na CHARLES WASONGA
MBUNGE wa Lari Jonah Mburu Mwangi amekamatwa Ijumaa pamoja na maafisa wanne wa Hazina ya Ustawi wa Eneo Bunge hili (CDF) kufuatia agizo la Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji.
Kwenye taarifa aliyoitoa, mbunge huyo anahutumiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya mamlaka na ufujaji wa Sh27 milioni za hazina hiyo.
“Mheshimiwa Jonah Mburu Mwangi na maafisa wa CDF walitumia vibaya mamlaka yao kwa kupokea fedha za umma kutoka kampuni ambazo zilipewa zabuni na hazina ya CDF ya eneobunge la Lari,” Haji akasema.
Maafisa wa hazina hiyo waliokamatwa na mbunge huyo ni; Ayaan Mahadhi (Meneja wa Hazina ya CDF, Lari), Peter Mugo Mwangi (Mwenyekiti wa CDF, Lari), Grace Muthoni Macharia (Mwanakandarasi) na Francis Gachoka Kamuyu (Karani wa Ujenzi, CDF, Lari)