• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Sakaja atozwa faini ya Sh15,000

Sakaja atozwa faini ya Sh15,000

Na JOSEPH WANGUI

SENETA wa Nairobi, Bw Johnson Sakaja jana alitozwa faini ya Sh15,000 baada ya kukiri mashtaka ya kukiuka amri ya kutotoka nje usiku na kukaidi kanuni za Wizara ya Afya za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Akiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Roselyne Onganya katika Mahakama ya Kasarani, Bw Sakaja alisema anajutia tukio hilo na tabia yake.

Alisema pia alikuwa ashaomba msamaha kwa Wakenya.Upande wa mashtaka ulieleza kwamba Bw Sakaja, pamoja na wengine, walikamatwa na polisi Ijumaa iliyopita wakifurahia vileo katika baa inayojulikana kama Ladies Lounge eneo la Kilimani.

Ripoti zingine zilionyesha kuwa Bw Sakaja alikuwa ametishia kusababisha uhamishaji wa maafisa wa polisi waliomkamata kufuatia tukio hilo.

Lakini alikanusha madai hayo na kusema yeye ni raia anayeheshimu sheria na hana mamlaka ya kuhamisha afisa yeyote.Bw Sakaja, kupitia wakili John Khaminwa, aliomba radhi kuhusiana na tukio hilo.

Wakili aliambia Mahakama kuwa, Bw Sakaja alikuwa tayari amekiri makosa yake hata kabla ya kushtakiwa.

You can share this post!

Matumaini ya mavuno licha ya janga la corona

‘Nzige watachangia utapiamlo katika jamii za wafugaji’

adminleo