• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:38 AM
Babayao akunja mkia kufuata Uhuru

Babayao akunja mkia kufuata Uhuru

Na MWANGI MUIRURI

ALIYEKUWA Gavana wa Kiambu, Bw Ferdinand Ndung’u Waititu amesalimu amri na kuamua kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na washirika wake ndani ya mrengo wa Kieleweke na handisheki.

Gavana huyo wa zamani anayefahamika kama Babayao alihudumu kati ya 2017 hadi Desemba 2019 ambapo alinga’tuliwa mamlakani Januari 2020 kwa madai ya ufisadi na utovu wa maadili.

Akihudhuria mkutano wa rais katika Ikulu ndogo ya Sagana Jumamosi, Bw Waititu ambaye awali alikuwa mfuasi na mtetezi sugu wa Naibu wa Rais Dkt William Ruto alisema kwa sasa ni vyema viongozi wa Mlima Kenya waungane.

Hii ni kinyume na awali aliposema hangemsaliti Dkt Ruto.

“Tumtii rais kama kiongozi wetu wa sasa na tumpe heshima anayohitaji kama kinara wa siasa zetu za Mlima Kenya,” akasema.

Bw Waititu aliungama kuwa ‘wakati mwingine sio vizuri kuzidisha vita na mirengo iliyo na nguvu na mara kwa mara ni suala la busara kuwapisha walio na nguvu.”

 

You can share this post!

Uhuru amsaga Ruto Sagana

Sina haja kulipwa deni 2022 – Ruto