• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 7:50 AM
TAHARIRI: Chanjo kwa wingi itasaidia kukabiliana na corona mpya

TAHARIRI: Chanjo kwa wingi itasaidia kukabiliana na corona mpya

Na MHARIRI

JUMA lililopita dunia ilishikwa na fadhaa nyingine baada ya kutangazwa kwamba virusi vipya vya korona vimeibuka tena.

Wanasayansi katika taifa la Afrika Kusini walitangaza kwamba baada ya uchunguzi wao katika maabara, walitambua virusi vya Omicron.

Hatua hii badala ya kupongezwa na dunia, ililetea taifa la Afrika Kusini adhabu kwani mataifa mengi ya ughaibuni yalipiga marufuku raia wa taifa hili kuzuru nchi zao.

Kwa kweli unyanyapaa huu haukufaa hata kidogo.

Afrika Kusini ilifaa kupongezwa kwa utafiti maabarani uliowezesha virusi vipya kupatikana.

Hatua hii itasaidia wataalamu kote duniani kuzama katika utafiti mwingine ili kutanzua tatizo linalokodolea ulimwengu macho.

Kile ambacho kimesababisha kiwewe katika dunia kuhusu virusi hivi ni kwamba, vina uwezo wa kuwapata hata watu waliojipatia kinga ya awali kutokana na maambukizi ya awali ya corona.

Hii ni kwa sababu virusi vya Omicron vina uwezo mkubwa wa kukwepa kinga-mwili tofauti na virusi vya awali kama vile Delta.

Nafuu ya pekee tu ni kwamba kwa wale watakaoambukizwa virusi vya Omicron na wawe tayari waliambukizwa corona awali, basi makali yatakuwa hafifu.

Hata hivyo, kufikia sasa wataalamu hawajabainisha makali ya virusi hivi vipya yatakuwaje kwa watu ambao tayari wamechanjwa.

Kutokana na ubayana huu wa awali ambao tumeupata kutoka kwa wataalamu, basi hatua ya busara kwa serikali zote za ulimwengu mbali na hatua nyinginezo inafaa kuhakikisha kwamba raia wake wanapata chanjo kwa wingi.

Watu waliochanjwa wana nafuu ikija katika maambukizi ya corona.

Bara la Afrika ndilo lenye mtihani mkubwa kukabili Omicron.

You can share this post!

Shujaa yarejea nyumbani na majeraha Kabras ikikwamilia juu...

Mkenya ashinda Fukuoka Marathon kwa mara ya kwanza tangu...

T L