• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 10:55 AM
Hedimasta ndani miaka 9 kwa kumeza hongo ya Sh10,000

Hedimasta ndani miaka 9 kwa kumeza hongo ya Sh10,000

Na Stephen Muthini

MKUU wa Shule ya Sekondari katika Kaunti ya Machakos amehukumiwa jela miaka tisa kwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh10,000.

Msimamizi huyo wa Shule ya Sekondari ya Wakaela, Bw Paul Nduve Silla alihukumiwa kwa kupokea pesa hizo ili aweze kutoa hundi ya malipo ya kompyuta na vifaa vingine husika.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mwandamizi Abdul Lorot, alisema ufisadi umekuwa shida kubwa nchini Kenya na kwamba unahitaji kukomeshwa.

“Ufisadi ni tatizo sugu katika nchi hii. Imekuwa kawaida katika taasisi zetu za umma na kuathiri maadili yetu. Wakati huu mahakama zitarejesha hali inayostahili katika nchi yetu,” alisema Bw Lorot. Mshtakiwa alikabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni pamoja na kuomba rushwa.

Mtego

Mshtakiwa huyo alinaswa baada ya kutegwa na Sh10,000 na kushtakiwa mnamo Februari 2014.

Hukumu zote zitaambatana na atahudumu jela miaka sita kwa jumla.

“Kutuma ujumbe dhabiti, mshtakiwa atatumikia miaka mitatu jela kwa kosa la kwanza, miaka mingine mitatu kwa kosa la pili na mitatu kwa kosa la tatu,” aliamuru hakimu.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo ana siku 14 kukata rufaa.

 

You can share this post!

SAKATA YA NYS: Wabunge wa Jubilee na Nasa wataka Waziri...

Jaji azima madaktari wa Cuba kuanza kuhudumu Kenya

adminleo