• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Ilani kwa wahudumu wa matatu kuhusu ukiukaji wa sheria jijini

Ilani kwa wahudumu wa matatu kuhusu ukiukaji wa sheria jijini

Na Collins Omulo

VYAMA vya mashirika ya usimamizi wa matatu (Sacco) zinazokiuka sheria jijini Nairobi vimepatiwa ilani kuhusu kuongezeka kwa matatu zinazobeba na kushusha wateja katika maeneo yaliyopigwa marufuku katikati mwa jiji kuu.

Hii ni baada ya madiwani wa Nairobi kutwika jukumu Halmashauri ya Utowaji Huduma Nairobi (NMS) la kuadhibu vituo vilivyowekwa kinyume na sheria, ambavyo vinahusishwa na mashirika ya mabwenyenye yanayoshirikiana na sacco za matatu.

Visa hivyo vinavyokiuka sheria vimeongezeka jijini na kuingilia nafasi zilizotengewa wamiliki biashara na madereva wa teksi huku barabara ya Tom Mboya Street ikitajwa kama iliyoathiriwa zaidi. Diwani wa Wadi ya Kati Daniel Ngegi alidai kuwa katika barabara ya Tom Mboya Street; matatu za Azuri, Surmount, Nazige na Embakasi Sacco zimefurusha teksi ambazo zimekuwa zikiendesha shughuli zake katika eneo hilo kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita, huku Circular Sacco ikianza kuendesha shughuli zake katika maeneo ya kibiashara nje ya Tuskys Supermarket.

Sacco nyingine tano zikiwemo Compliant, Madiwa, Jesmat, Travelmatt na MMOG pia zimemulikwa kwa kuendesha shughuli zake kinyume na sheria kwenye makutano ya barabara ya Sheikh Karume na kufunga barabara.

??????

  • Tags

You can share this post!

Bunge la Uganda laandikisha visa 200 vya maambukizi ya...

West Brom wapata kocha mpya kizibo cha Sam Allardyce