• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Jirongo akubaliwa kusafiri Sudan Kusini

Jirongo akubaliwa kusafiri Sudan Kusini

Na RICHARD MUNGUTI

MWANIAJI kiti cha Urais aliyeshindwa 2017 Cyrus Jirongo anayekabiliwa na ufisadi wa Sh50 milioni amerudishiwa pasipoti yake kumwezesha kusafiri hadi Sudan kusini kusimamia biashara zake.

Hakimu mkuu Francis Andayi alisema ni haki ya kila mwananchi kusafiri pasi kuwekewa masharti.

Bw Andayi alimwamuru Bw Jirongo aliyekana mashtaka manne afike tena mahakamani Oktoba 11 kueleza hajatoroka.

Wakili Dunstan Omari (kulia), Bw Jirongo (kati) na wakili Bernard Koyoko wazungumza baada ya kesi dhidi ya mwanasiasa huyo katika mahakama ya Milimani. Picha/ Richard Munguti

Mbunge huyo wa zamani wa Lugari alikanusha shtaka la kuilaghai benki ya Post Bank Credit Sh50m kwa kuipa hatimiliki ya shamba la Sammy Kogo.

Pia ameshtakiwa kwa kutoa habari za uwongo kwa polisi kwamba alikuwa amempa marehemu Jonathan Moi Sh7 milioni, kati ya pesa hizo zilizofujwa benki ya Post Bank Credit Ltd kumnunulia kampuni ya Soy Developers.

You can share this post!

Chapa Dimba ilivyomfungulia David Majak milango ya heri

Wanaoshukiwa kuiba Sh75m waachiliwa kwa Sh1m kila mmoja

adminleo