• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:25 PM
K.U yapoteza mamilioni baada ya TZ na Rwanda kufunga mabewa yake

K.U yapoteza mamilioni baada ya TZ na Rwanda kufunga mabewa yake

Na BERNARDINE MUTANU

CHUO Kikuu cha Kenyatta kimepoteza Sh518 milioni kilichotumia kuanzisha mabewa Kigali na Arusha, baada ya serikali za Rwanda na Tanzania kufunga mabewa hayo.

Chuo hicho kilitumia Sh420, 749,207 kuanzisha bewa la Kigali na Sh97, 425,152 kujenga bewa la Arusha.

Kulingana na mchunguzi mkuu wa hesabu za serikali Edward Ouko, chuo hicho kilifunga mabewa hayo kutokana na changamoto za utekelezaji wa huduma.

Hii ni baada ya serikali za Rwanda na Tanzania kubadilisha sheria baada ya KU kukamilisha matakwa yote na kuwa tayari kuzindua programu zake katika mabewa hayo.

“Ingawa chuo hicho kilielezea kuwa taratibu zote zilifuatwa kabla ya uamuzi kufanywa kufungua mabewa hayo mawili, usimamizi haujaeleza hatua unazotekeleza kupata pesa zote zilizotumika ambazo ni Sh518, 174, 359,” alisema katika ripoti ya ukaguzi wa vitabu vya chuo hicho vya mwaka wa kifedha uliokamilika Juni.

Kamati ya bunge kuhusu uwekezaji wa umma (PIC) katika ripoti 2016, KU ilifungua mabewa hayo bila kuzingatia idhini kutoka taasisi husika Nairobi na Kigali.

You can share this post!

Mswada wa NYS kuwasilishwa bungeni

Jopo lateuliwa kupima mamlaka ya DPP

adminleo