• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:30 PM
Leba Dei 2023: Askofu asuta Raila Odinga kupitia maombi

Leba Dei 2023: Askofu asuta Raila Odinga kupitia maombi

Na TITUS OMINDE

ILIKUWA kinaya kwa kiongozi wa kidini Askofu mstaafu Arthur Kitonga kutumia fursa ya kutoa maombi wakati wa sherehe ya maadhimisho ya Leba Dei 2023 katika bustani ya Uhuru, kukemea upinzani.

Askofu Kitonga ambaye alipaswa kunukuu Bibilia wakati wa maombi, badala yake alitumia jina la kiongozi wa upinzani Raila Odinga, huku akimkejeli.

Maombi ya askofu Kitonga yalichukua mkondo wa malumbano ya kisiasa alipoanza kukashfu mipango ya upinzani kuandaa maandano kote nchini.

“Mambo ya mapambano barabarani kwa watu kuharibu biashara ya watu tunaikataa katika jina la Yesu,” alitamka askofu Kitonga huku akionekanana kufokea Bw Odinga.

Kiongozi huyo wa kidini ambaye alionekana kusifu Rais William Ruto, badala ya Mungu aliendelea kukemea Bw Odinga.

Askofu Kitonga alikemea upinzani kisema “tunaomba Raila Odinga akome kushiriki maandamano na azeeke vyema.”

Ajabu ni kwamba badala ya kiongozi huyo kunukuu sehemu ya Bibilia kwa maombi yake, aliamua kunukuu majina ya viongozi wa kisiasa.

“Tunamuombea kiongozi wa upinzani mheshimiwa Raila Odinga azeeke na kustaafu kwa amani, wakati huu ni wa uongozi wa Bw Ruto aliyechakuliwa vyema,” alisema Kitonga

Mbali na kutaka Bw Odinga astaafu vyema askofu Kitonga pia alitumia fursa hiyo kutaka Bw Odinga kuachana na mambo ya maandamano huku akishangiliwa na umati uliokuwa katika bustani ya Uhuru.

Askofu Kitonga alisifu Rais Ruto kama kiongozi ambaye alipakwa mafuta na Mungu.

“Kazi hii ya uongozi ulimpatia Bw Ruto aendelee na hatutaki kuona malumbano kuanzia leo, siku hii ya Leba Dei,” alisema askofu Kitonga.

Isitoshe, kiongozi huyo hakunukuu fungu lolote la Bibilia katika maombi yake.

  • Tags

You can share this post!

Wahubiri North Rift: Tuko tayari kupigwa msasa

Ajabu watu 2 pekee wakihudhuria sherehe ya Leba Dei Eldoret...

T L