• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Mabroka kuendelea kuvuna serikali ikitangaza bei ‘duni’ ya kununua mahindi

Mabroka kuendelea kuvuna serikali ikitangaza bei ‘duni’ ya kununua mahindi

NA RICHARD MAOSI

Waziri wa Kilimo Mithika Linturi ametangaza kwamba serikali itanunua gunia la kilo 90 la mahindi kutoka kwa wakulima kwa Sh4,000.

Anasema ni mojawapo ya mikakati ili kuwalinda dhidi ya mabroka ambao wamekuwa wakiwapunja kwa kununua mahindi kwa bei ya chini na kuuza ghali.

Waziri Linturi alikuwa akizungumza katika Taasisi ya Ndomba ambayo hutoa mafunzo kuhusu Ustawishaji Afya ya mifugo.

Hata hivyo, ni jambo ambalo halijapokelewa vyema ikizingatiwa wakulima wa mahindi kutoka Kaunti ya Uasin Gishu, kwa mfano, wanauza gunia la kilo 90 ya mahindi baina ya Sh4,400-4,600.

Ikiwa ni bei ya chini ikilinganishwa na awali ambayo ilikuwa kati ya Sh5,000-5,200.

Aidha, uchunguzi wa Taifa Leo unaonyesha kuwa katika maeneo ya Ziwa, Kapsabet, Itigo, Kapsabet, Nandi Hills na Kitale, bado wakulima wanategemea mabroka ili mazao yao kupata soko.

Hatua ya Wizara ya Kilimo kutangaza bei ya mahindi inajiri siku chache tu baada ya wakulima kutoka Kaunti za Trans Nzoia, Uasin Gishu na Nandi kulalamikia serikali iwanunulie mahindi ambayo yalikuwa yanaharibikia shambani.

Kuanzia Septemba msimu wa mvua nyingi ulifanya baadhi yao kuuza mazao kwa bei ya kutupa kwa sababu ya ukosefu wa mbinu sahihi za kuhifadhi mazao.

Masaibu mengineyo yakiwa ni pamoja na  gharama kubwa ya pembejeo za kilimo na kuongezeka kwa bei ya mafuta ambayo kwa asilimia kubwa ilisababisha kupanda kwa gharama ya uzalishaji.

  • Tags

You can share this post!

Seneta mwenye ulemavu wa macho asisimua kwa kuzindua albamu...

Mwanamke asimulia alivyoponyoka na wanawe mauti Shakahola...

T L