• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 PM
Maguire aambiwa unahodha hautampa uhakika wa kuunga kikosi cha kwanza cha Man-United

Maguire aambiwa unahodha hautampa uhakika wa kuunga kikosi cha kwanza cha Man-United

Na MASHIRIKA

KOCHA Eric ten Hag wa Manchester United amemsifu beki Raphael Varane na kusisitiza kuwa utepe wa unahodha si kigezo kitakachompa difenda Harry Maguire uhakika wa kuunga kikosi cha kwanza cha mabingwa hao mara 20 wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Maguire ambaye amehusishwa na uwezekano wa kujiunga na Chelsea, alitemwa katika kikosi kilichotegemewa na Ten Hag kupepeta Liverpool 2-1 mnamo Agosti 2022 uwanjani Old Trafford.

Badala yake, Varane aliaminiwa kushirikiana na sajili mpya Lisandro Martinez katika safu ya ulinzi ya Man-United na Mfaransa huyo aliyetokea Real Madrid mnamo 2021-22 akaridhisha pakubwa.

“Mchango wa Varane dhidi ya Liverpool ulikuwa mkubwa. Aliwanyima wapinzani wetu nafasi nyingi za kuvurumisha makombora mazito langoni. Alijituma vilivyo, akaongoza kikosi ipasavyo na kudhihirisha kiu ya kutaka kushinda mechi,” akasema Ten Hag.

Maguire alipangwa katika kikosi cha kwanza cha Man-United kilichotandikwa na Brighton 2-1 ugani Old Trafford na katika kikosi kingine kilichopondwa na Brentford 4-0 ugenini.

Maguire aliyesajiliwa kutoka Leicester City alilengwa na mashabiki wa Man-United uwanjani mara kadhaa mnamo 2021-22 huku akizomewa, kurushiwa cheche za maneno na kutishiwa maisha wakati wa mechi ya kirafiki iliyokutanisha Man-United na Crystal Palace nchini Australia mnamo Julai 2022.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Everton wapata mfumaji wa kujaza pengo la Richarlson...

WALIOBOBEA: Nyota ya Kituyi ilianza kung’aa akiwa chuoni

T L