• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 12:45 AM
Michael Joseph ateuliwa mwenyekiti wa bodi ya Safaricom

Michael Joseph ateuliwa mwenyekiti wa bodi ya Safaricom

Na PAUL WAFULA

KAMPUNI ya mawasiliano ya Safaricom imemteua afisa wao wa zamani Michael Joseph kama mwenyekiti mpya wa bodi yake.

Bw Joseph alichukua wadhifa huo kutoka kwa Nicholas Ng’ang’a ambaye amekuwa uongozini tangu 2007, akiwa amehudumu kwa miaka 13.

Vilevile Bw Ng’ang’a amekuwa kwenye bodi ya Safaricom, kwa muda wa miaka 16 baada ya kujiunga kama mwanachama mnamo 2004.

Akitangaza uteuzi huo, Afisa Mkuu Mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa amesema Bw Joseph atachukua wadhifa huo rasmi Agosti 1, 2020, huku jukumu lake kubwa likiwa kujenga brandi ya kampuni na kuivumisha ili iendelee kupata faida.

“Ana ujuzi na ufahamu pana kwa kuwa mchango wake kwenye makuzi ya Safaricom kutoka kampuni ya kawaida hadi ile yenye mapato zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki,” akasema Bw Ndegwa.

Bw Joseph anaelewa sana Safaricom kuwa kuwa alihudumu kama afisa mkuu mtendaji mara mbili na pia mwanachama wa bodi yake kwa miaka kadhaa.

Wakati wa uongozi wake ndipo Safaricom ilizindua mfumo wa kutuma na kupokea fedha maaarufu kama Mpesa ambayo imenufaisha wengi duniani.

You can share this post!

Mahakama yaagiza SABIS® International ipunguze karo kwa...

Kinara wa Team Kenya michezo ya Olimpiki 2016 ajitetea...

adminleo