• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Misri, Ghana mawindoni kufukuzia nafasi ya kuingia AFCON 2023

Misri, Ghana mawindoni kufukuzia nafasi ya kuingia AFCON 2023

NA MASHIRIKA

MISRI wataanza kuwinda nafasi ya kunogesha fainali za Kombe la Afrika (AFCON) nchini Ivory Coast mnamo 2023 kwa kualika Guinea leo katika pambano la Kundi D jijini Cairo.

Kwingineko, Ghana waliokung’uta Bukini 3-0 katika mchuano wa ufunguzi wa Kundi E mnamo Jumatano ugani Cape Coast Sports, wataendea Central African Republic (CAR) uwanjani Estadio 11 de Novembro.

CAR ambao hawajashinda mechi yoyote kati ya sita zilizopita tangu walaze Nigeria 1-0 mnamo Oktoba 2021, watashuka ugani wakipania kujinyanyua baada ya Angola kuwapiga 2-1.

Motisha yao itachochewa na rekodi duni ya Ghana ambao wameshinda mechi moja pekee kati ya 12 zilizopita ugenini tangu 2020.

The Pharaohs waliokosa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2022 baada ya Senegal kuwazima kwa penalti mnamo Machi, watashuka dimbani wakijivunia rekodi ya kutoshindwa katika mechi 10 mfululizo katika uwanja wa nyumbani.

Miamba hao wnaaojivunia mataji saba ya AFCON, wameshinda michuano tisa na kuambulia sare mara moja tangu wapokezwe kichapo cha 1-0 kutoka kwa Afrika Kusini mnamo Julai 2019.

Chini ya kocha Ehab Galal, Misri watakuwa na kiu ya kuendeleza ubabe dhidi ya Guinea ambao wamepoteza mara tatu na kuambulia sare mara moja kutokana na mechi nne zilizopita dhidi yao.

Guinea walicheza mara ya mwisho mnamo Machi 25 katika mchuano wa kirafiki uliokamilika kwa sare tasa kati yao na Afrika Kusini uwanjani Guldensporen, Ubelgiji.

Hiyo ilikuwa baada ya Gambia kuwang’oa katika raundi ya 16-bora kwenye fainali za AFCON mnamo Januari nchini Cameroon.

Guinea hawajashinda mechi yoyote kati ya nne zilizopita katika mashindano yote huku wakitoka sare mara mbili na kupoteza mara mbili tangu wapepete Malawi 1-0 katika pambano la hatua ya makundi ya AFCON mnamo Januari 10.

Kikosi hicho cha mkufunzi Kaba Diawara kinatazamia kushiriki fainali za AFCON kwa mara ya tatu mfululizo, kwa mara ya pili katika historia.

Misri watategemea zaidi maarifa ya mshambuliaji Mohamed Salah wa Liverpool anayeshikilia nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote kambini mwao kwa mabao 47 kutokana na mechi 82.

RATIBA YA KUFUZU AFCON 2023 (Leo Jumapili):

Malawi va Ethiopia (4:00pm)

Bukini vs Angola (4:00pm)

CAR vs Ghana (4:00pm)

Botswana vs Tunisia (4:00pm)

Misri vs Guinea (10:00pm)

  • Tags

You can share this post!

FATAKI: Mabinti kufuata pesa ni sawa ila wasikae tu ndee...

Nitabwaga Raila Agosti, asema Ruto

T L