• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 1:29 PM
Nakuru City Queens wanyorosha Ulinzi Starlets, Zetech Sparks ikisagasaga Kayole

Nakuru City Queens wanyorosha Ulinzi Starlets, Zetech Sparks ikisagasaga Kayole

AREGE RUTH Na OSBORN MANYENGO

WANAJESHI wa Ulinzi Starlets walipoteza mechi ya kwanza nyumbani jana Jumapili, waliponyoroshwa 3-1 na Nakuru City Queens katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake (KWPL) iliyochezwa ugani Ulinzi Sports Complex, Nairobi.

Dakika za kwanza 10 za mchezo, timu zote zilionekana kutoshana nguvu. Nakuru walipata nafasi ya kufunga dakika ya nne kupitia kona ya Elizabeth Muteshi lakini haikuzaa matunda.

Ulinzi nao walipata nafasi ya kufunga dakika mbili baadae lakini mpira wa kona kutoka kwa Lucy Nato, lakini kipa wa Nakuru Juliet Adhiambo alikuwa amemakinika kwenye lango.

Kasi ya mchezo ilipoendelea kupanda, wanajeshi walicheka na wavu wa kwanza dakika ya 13 kupitia nahodha Sheryl Angachi baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Nakuru.

Muteshi alisawazisha bao dakika ya 21. Kiungo Stacy Koech aliongeza bao la tatu dakika ya 76. Ruth Chebungei alifunga kazi dakika ya 89 kupita penalti baada ya kipa Belinda Akinyi kumchezea visivyo kwenye kijisanduku.

“Waliiingia mchezoni wakiwa na woga mwingi. Hili lilichangia kufungwa bao la mapema. Kushinda mechi dhidi ya Ulinzi sio jambo rahisi, ushindi huu umeleta morale kwenye timu yangu,” alisema kocha wa Nakuru Chris Wesonga.

Mwenzake wa Ulinzi Joseph Mwanzia, alinyoosha kidole cha lawama kwa kipa Akinyi ambaye alisema hakumakinika kwenye lango.

Ugani Gems Cambridge, Zetech Sparks waliwanyorosha Kayole Starlets 5-0.

Mshambuliaji Puren Alukwe alifunga mabao mawili, Violet Achieng, Monalisa Achieng na Yvonne Kavere wakafunga bao kila mmoja.

Mabingwa mara tatu Vihiga Queens waliendelea kung’aa kwenye ligi baada ya kulima Kisumu Allstarlets mabao 2-0, katika uwanja wa Mumias Complex.

Magoli ya Vihiga yalifungwa Anita Namata na Janet Moraa Bundi dakika ya 18 na 64 mtawalia.

“Muhimu ni alama sio mabao tukishinda hata kwa bao moja pekee ni muhimu kwetu,” alisema kocha wa Vihiga Boniface Nyamuhnyamuh.

Kwingineko, Bunyore Starlets walitoshana nguvu ya 0-0 na Gaspo Women ugani Mumboha.

  • Tags

You can share this post!

Arsenal wakomoa Man-United uwanjani Emirates na kuendeleza...

MWALIMU WA WIKI: Njuguna ni mwalimu mwenye kiu ya utafiti

T L